Anna Margareth Abdallah

Anna Margareth Abdallah (alizaliwa 26 Julai 1940) ni mwanasiasa wa Chama cha Mapinduzi na aliwahi kuwa mbunge wa viti maalumu kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi mwaka 2015.[1]

Anna Abdallah Mbunge

tarehe ya kuzaliwa 26 Julai 1940 (1940-07-26) (umri 84)
Tanganyika

Maisha

hariri

Anna Margareth Abdallah alipata shahada yake ya kwanza ya mambo ya sosholojia katika chuo kikuu cha Missouri (University of Missouri) kilichopo huko Columbia nchini Marekani mnamo mwaka 1963.[2]

Mwaka 1967 alipata diploma yake ihusuyo Uchumi wa nyumbani (kiing.Home Economics) kutoka Chuo kikuu cha London kilichopo Uingereza.[3]

Abdallah ni mwanachama wa chama tawala CCM. Aliwahi kuwa mbunge kwa mara yake ya kwanza mnamo mwaka 1975, ambapo kwa wakati huo kulikuwa na wabunge wanawake watano tu katika bunge zima la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.[4] A qualified nurse,[5]

Abdallah pia aliwahi kuwa Waziri wa Afya kwa kipindi cha 2000-2005[6]

Nyadhifa nyingine za serikali alizowahi kuzifanyia kazi ni pamoja na Waziri wa Kazi (1995-200), Waziri wa maendeleo ya kilimo na mifugo (1991) na waziri wa serikali za mitaa, maendeleo ya jamii na masoko shirikishi.[7]

Pia Abdallah alikuwa ndiye mwanamke wa kwanza kuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.[4].Aliwahi pia kuwa mwenyekiti wa umoja wa wanawake watanzania kutoka mwaka 1994-2008.[7][2]

Mnamo mwaka 1991, alisaidia kuhamasisha mtandao wa watu watengeneza amani (Creators of Peace (CoP)) katika mkutano uliofanyikia Hotel ya Caux (conference centre in Caux) nchini Uswisi.Mtandao huo ulikuwa ni mkubwa ulimwenguni kote wenye uliowataka watu kila mmoja kuwa na kaulimbiu ya kutengeneza amani popote tulipo,mioyoni mwetu,nyumbani mwetu,mahali tufanyiapo kazi na katika jamii’’.Tangu hapo mtandao wa CoP umekua ukienea katika mataifa mbalimbali duniani hasa katika bara la Afrika ambapo nchi za (Afrika Kusini, Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda, Sudani Kusini, Sudan, Cameroon, Nigeria, Tanzania n.k) ni miongoni mwa nchi zinazo unga mkono na kuendeleza mtandao huo.

Marejeo

hariri
  1. "Member of Parliament CV". Parliament of Tanzania. 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Aprili 2013. Iliwekwa mnamo 14 Septemba 2013. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 Sheldon, Kathleen (2016-03-04). Historical Dictionary of Women in Sub-Saharan Africa (kwa Kiingereza). Rowman & Littlefield. ISBN 9781442262935.
  3. "Members Profile >> MP CV". Parliament of Tanzania website. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-12-03. Iliwekwa mnamo 2007-08-04. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  4. 4.0 4.1 Smith, David. "Anna Margareth Abdallah: 'They say, "Don't vote for the woman, she wears lipstick"'", The Observer, 2014-02-09. (en-GB) 
  5. "Ex-minister stays tight-lipped over AIDS drug controversy", This Day, 2007-03-08. Retrieved on 2007-08-04. Archived from the original on 2007-09-28. 
  6. "Welcome Note by Minister of Health". United States Embassy in Tanzania. 2005-10-10. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-09-22. Iliwekwa mnamo 2007-08-04.
  7. 7.0 7.1 O'Neil, Maureen (2003). "Diseases Without Borders: An Economic Struggle?". International Development Research Centre. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-05-17. Iliwekwa mnamo 2007-08-04. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Anna Margareth Abdallah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.