Ansberto wa Rouen (pia: Auedebati, Autbati, Autbertus; Chaussy-sur-Epte, leo nchini Ufaransa, karne ya 7Hautmont, 695 hivi) alikuwa askofu wa Rouen (Ufaransa) miaka 683 - 690.

Mt. Ansberto katika dirisha la kioo cha rangi katika kanisa kuu la Rouen.

Baada ya kushika vyeo vikubwa katika ikulu alijiunga na monasteri chini ya kanuni ya Kolumbani na miaka sita baadaye akawa abati. Hatimaye alifanywa askofu hadi alipoondolewa na Meya wa ikulu akarudia maisha ya monasterini[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Februari.[2]

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.