Antoni Kim Songu

(Elekezwa kutoka Antoni Kim Song-u)

Antoni Kim Songu (alifariki Tangkogae, 29 Aprili 1841) alikuwa Mkristo wa Korea aliyezoea kukusanya waumini wenzake wengi nyumbani mwake hadi aliponyongwa gerezani kwa ajili hiyo.

Ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakatoliki wa nchi hiyo waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 17911888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.

Yeye na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[1]

Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 29 Aprili[2].

Mazingira hariri

Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[3] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[4].

Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. "Korea and the church of martyrs". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-25. Iliwekwa mnamo 2020-04-07. 
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
  3. Michael Walsh, ed. "Butler's Lives of the Saints" (HarperCollins Publishers: New York, 1991), p. 297.
  4. The Liturgy of the Hours Supplement (New York: Catholic Book Publishing Co., 1992, pp. 17–18.

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.