Aso ebi mara nyingine huandikwa hivi Asoebi/Ashoebi kwa Kinaigeria, na Ashobie kwa Sierra [1] na Gambia [2] Ni aina ya vazi la kitamaduni la nchini Nigeria na tamaduni nyingine za Kiafrika likiashiria ushirikiano, urafiki na mshikamano wakati wa sherehe, hafla na matukio.[3]. Dhumuni la kuvaa vazi hilo ni kutumika na kujitambulisha katika kundi la rika moja,jamaa au marafiki wakati wa hafla za kijamii au mazishi.Upatikanaji wa vitambaa kama vile Ankara umechangia umaarufu wa uvaaji wa sare hizo kwa hafla za kijamii kwenye utamaduni wa Kiyoruba na Nigeria kwa jumla.

Kikundi kikiwa katika vazi la Aso ebi Nigeria
Wanawake wa Ivori wakiwa katika vazi la Aso ebi

Marejeo

hariri
  1. "Adding color". On mission Sierra Leone Blog (kwa Kiingereza). 2011-11-29. Iliwekwa mnamo 2022-03-16.
  2. "Fashion & Culture/The Cultural Value of the "Ashobie" :: My Basse ~". www.friendsofbasse.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-10-16. Iliwekwa mnamo 2022-03-16. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  3. "Aso ebi", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-02-21, iliwekwa mnamo 2022-03-16