Atasamale
Atasamale (pia Tesmalo) alikuwa mama wa mfalme wa Nubia Harsiotef (aliyeongoza karibu mwaka 400 KK). Anajulikana kutokana na stela ya mwanae na mazishi yake huko Nuri. Sifa yake ni mama wa wafalme, dada wa mfalme na Bibi wa Kush.[1] Huenda alikuwa mke wa Amanineteyerike, ingawa hii ni kuhisi tu.
Mazishi yake huko Nuri yalikuwa ya piramidi na kanisa dogo na vyumba viwili vya mazishi chini ya ardhi. Kulikuwa na ngazi zilizokuwa zikiingia ardhini na kuelekea kwenye vyumba viwili. Piramidi ilipatikana ikiwa imevunjwa, lakini vipande vya shabti ambavyo havikuwa na maandishi vilipatikana. Kulikuwa na vyombo kadhaa na kete iliyotengenezwa kwa fayansi au pasta nyeupe. Jina lake lilihifadhiwa kwenye meza ya kutoa dhabihu iliyopatikana hapo.[2]
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Atasamale kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |