Azteki ilikuwa jina la ustaarabu muhimu nchini Mexiko kabla ya kufika kwa Wahispania. Waazteki walitawala nyanda ja juu za Mexiko ya Kati pamoja na mji mkuu Tenochtitlan uliokuwa Jiji la Meksiko jinsi uanvyoitwa leo.

Milki za Mexiko wakati wa kufika kwa Wahispania 1519

Asili ya Azteki

hariri

Waazteki ambai kiasili walikuwa wavindaji na wahamiaji walifika mnamo mwaka 1325 kwenye ziwa la Texcoco kutoka kaskazini wakajenga makazi yao kwenye kisiwa ziwani wakaita mji "Tenochtitlan".

 
Askari Azteki; kengee za mikuki inakata kwa vipande vikali vya mawe magumu

Upanuzi wa utawala

hariri

Wafalme wa Azteki walipanusha eneo lao na hadi kufika kwa Wahispania mji mkuu ulikuwa na wakazi 300,000 ukiwa mji mkuu wa milki iliyotawala maeneo mapana katika nyanda za juu. Kitovu cha milki hii kilikuwa maungano ya miji mitatu ya Tenochtitlan, Texcoco na Tlacopan.

Mji mkubwa wa Tenochtitlan ulilishwa kwa kodi za maeneo yaliyotawaliwa na Waazteki. Mtindo wa utawala huo ulikuwa kudai malipo ya kodi baada ya kuwashinda majirani. Menginevyo mila, desturi na sheria ziliendelea kufuatana na utamaduni wa kila mahali.

Mtindo huu ulirahisihsa utawala kwa sababu uliwaachia watawaliwa kiwango kikubwa cha uhuru wa ndani lakini baadaye ilikuwa rahisi kwa Wahispania kupasua milki hii kwa kujiunga na vikundi vilivyotawaliwa.

Jamii ya Waazteki ilikuwa na tabaka nne: Makabaila (tecuhtin), Wakulima (macehualtin), Wafanyabiashara (pochteca) na watumwa (tlatlacotin).

Kila Azteki alitakiwa kushiriki katika jeshi. Wengine walikuwa wanajeshi hasa bila kazi nyingine na hii ilikuwa njia ya kupanda ngazi katika jamii.

Kilimo

hariri

Kilimo cha Waazteki kilitumia mazao kama vile mahindi, maharagwe, mboga na nyanya. Hawakufuga wanyama isipokuwa mbwa na kuku lakini maziwa ya nyanda za juu yaliwapa samaki. Mazao mengi yaliyo kawaida leo hii duniani yaligunduliwa na kustaawishwa na wakulima wa Amerika kabla ya kufika kwa Wahispania.

Teknolojia

hariri

Teknolojia ya Azteki haikugundua bado matumizi ya chuma au shaba. Vifaa vyote vilikuwa vya ubao na mawe. Kwa visu na silaha walitumia mawe magumu sana ya obsidiani yaliyovunjwa na kuwa na kona kali. Silaha hizi hazikuweza kushindana na panga na kinga za chuma za Wahispania waliokuwa pia na aina za bunduki.

 
Kalenda ya Azteki

Mwisho wa ustaarabu

hariri

Mwaka 1519 alifika Mhispania Hernan Cortes pamoja na jeshi ya askari 450 kutoka visiwa vya Karibi vilivyovamiwa na Hispania tangu siku za Kristoforo Kolumbus. Baada ya kupokelewa vizuri na mfalme wa Azteki Moctezuma II walimkamata mfalme kama mfungwa na kuchukua dhahabu kutoka mahekalu. Wenyeji wa mji waliwashambulia na kuua Wahispania wengi. Cortes aliweza kukimbia akarudi na jeshi mpya akaweza kuteka mji tar. 13 Agosti 1521 na kuuharibu kabisa.

Kuja kwa Wazungu kulisababisha vifo vingi hasa kutokana na magonjwa yasiyojulikana bado Amerika bara lakini pia kutokana na vita na utumwa.

Huo ulikuwa mwisho wa ustaarabu wa Azteki.

  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Azteki kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.