Bamako ni mji mkuu wa Mali pamoja na kuwa mji mkubwa nchini ikiwa na wakazi milioni moja na nusu. Iko mwambaoni wa mto Niger katika kusini ya nchi.

Jiji la Bamako
Nchi Mali
Mkoa Bamako Capital District
Bamako na mto Niger
Bamako nchini Mali
Bamako kutoka mlimani
Watu huchunguza takataka Bamako
Watu huchunguza takataka Bamako

Historia hariri

Bamako ilianzishwa kama mji katika karne ya 17 BK na machifu wa kabila la Niare Seribadian Niaré na Soumba Coulibaly. Jina la asili lilikuwa "Bammako" (Kibambara: "bwawa la mamba"). Bamako ilikuwa soko muhimu pamoja na mji wa elimu ya Kiislamu katika Dola la Mali. Wakati wa karne ya 19 sifa zake zilikuwa zimepungua. Mwaka 1883 Wafaransa walikuta kijiji kikubwa cha watu 600 chenye kuta za ulinzi.

Wakati wa ukoloni Bamako ikawa makao makuu ya koloni la Senegal ya Juu-Niger mwaka 1899 halafu mji mkuu wa Sudan ya Kifaransa mwaka 1920. Ikulu ya Koulouba ilijengwa 1907 kama makao makuu ya gavana ikawa ikulu ya rais baada ya uhuru.

Mwaka 1904 Bamako iliunganishwa na reli ya Dakar - Niger. Majengo mengine ya siku zile yalikuwa kanisa kuu la katoliki mwaka 1927, daraja la kwanza juu ya mto Niger 1947 na misikiti mkuu mwaka 1948.

Mwaka 1955 Bamako ilipewa cheo cha mji kufuatana na sheria ya kifaransa. Meya mwafrika wa kwanza alikuwa Modibo Keïta mwaka 1956.

Tarehe 22 Septemba 1960 Mali ikapata uhuru wake Bamako ikawa mji mkuu wa jamhuri.

Majengo hariri

Majengo mazuri mjini ni maktaba ya kitaifa, mnara ya Tour BCEAO, msikiti kuu na daraja la mfalme Fahd (Pont du Roi Fahd). Hata makumbusho ya kitaifa, makumbusho ya Muso Kunda, makumbusho ya mkoa wa Bamako, zoo ya Bamako na kilima cha "Point G" chenye uchoraji wa mwambani zinapendeza vilevile.

Kuna uwanja wa ndege cha kimataifa na reli ya kwenda Koulikoro katika mashariki ya Mali na Dakar (Senegal).

Hara za mji hariri

 
Matatu au daladala za Bamako huitwa "sotruma"
  • Hippodrome.
  • Niarela.
  • Korofina.
  • Badalabougou.
  • Torokorobougou
  • Bamako Coura.
  • Djicoroni.
  • Baco Djicoroni (= ng'ambo ya mtoni).
  • Missira.
  • Médina Coura.
  • Bankoni.
  • Magnambougou.

Viungo vya Nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: