Baraza la mawaziri Tanzania
Baraza la Mawaziri la Tanzania ni ngazi ya juu ya serikali au mkono wa utendaji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mfumo wa mgawanyo wa madaraka.
Baraza hili linaundwa na rais, makamu wa rais, rais wa Zanzibar, waziri mkuu na mawaziri wote wanaoongoza moja ya wizara za serikali . [1] Manaibu mawaziri si sehemu ya baraza. Mwanasheria Mkuu anashiriki katika mikutano ya baraza lakini hana haki ya kupiga kura katika mikutano hiyo.
Mikutano ya baraza huongozwa na Rais kama mwenyekiti, kama Rais hayupo basi mikutano hiyo huongozwa na Makamu wa Rais, na kama wote wawili hawapo mikutano hiyo huongozwa na Waziri Mkuu.[2]
Serikali iliyopo ilitangazwa na John Pombe Magufuli, rais wa sita wa Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 mnamo tarehe 6 Desemba 2020,HADI 2021 Mwezi March Rais Magufuli alifariki Dunia kwa Corona. Kuanzia March 2021 Serikali inaongozwa Na Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa Msaidizi wake,Yaani Makamu wa Rais
Chama anachotoka | Chama Cha Mapinduzi |
---|
Marejeo
hariri- ↑ "Cabinet of Tanzania". tanzania.go.tz. May 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-04-18. Iliwekwa mnamo May 2012.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help); Italic or bold markup not allowed in:|publisher=
(help) - ↑ "Katiba ya Tanzania, fungu 54" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2010-12-17. Iliwekwa mnamo 2020-12-06.
- ↑ Baraza la mawaziri la Magufuli hili hapa, gazeti la Mwananchi tar 05.12.2020
Tazama pia
hariri