Baraza la mawaziri Tanzania 2015

Baraza la Mawaziri la Tanzania ni ngazi ya juu ya serikali au mkono wa utendaji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mfumo wa mgawanyo wa madaraka.

Baraza hili linaundwa na rais, makamu wa rais, rais wa Zanzibar, waziri mkuu na mawaziri wote. [1] Manaibu mawaziri si sehemu ya baraza. Mwanasheria Mkuu anashiriki katika mikutano ya baraza lakini hana haki ya kupiga kura katika mikutano hiyo.

Mikutano ya baraza huongozwa na Rais kama mwenyekiti, kama Rais hayupo basi mikutano hiyo huongozwa na Makamu wa Rais, na kama wote wawili hawapo mikutano hiyo huongozwa na Waziri Mkuu.[2]

Serikali iliyotangazwa na John Magufuli, rais wa tano wa Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 mnamo tarehe 10 Desemba 2015. Isipokuwa nafasi 4 zilichelewa kutajwa majina hadi tarehe 23 Desemba, na hapo waliingia Jumanne Maghembe, Philip Mpango, Gerson Lwenge na Joyce Ndalichako. Siku hiyohiyo Makame Mbarawa alihamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Chama anachotoka Chama Cha Mapinduzi
Baraza la mawaziri la Tanzania: mwishoni mwa mwaka 2015[3][4][5]
Picha Majukumu Jina
John Magufuli 2015.png Raisi
Amiri jeshi mkuu
Dr. John Magufuli
Samia Suluhu Hassan.jpg Makamu wa Rais Samia Suluhu
Ali Mohamed Shein, September 2014 (cropped).jpg Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein
Kassim Majaliwa.jpg Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Faili:Abdallah Ulega.jpg Kilimo Abdallah Hamis Ulega
No image.svg Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi
TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
Selemani Said Jafo
Angellah Kairuki.jpg Madini Angellah Kairuki
January Makamba 2012.jpg Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais
Masuala ya Muungano, Mazingira
January Makamba
No image.svg Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
Jenista Mhagama
No image.svg Mifugo na Uvuvi Luhaga Joelson Mpina
No image.svg Sheria na Katiba Professor. Paramagamba John Aidan Mwaluko Kabudi
Hussein Mwinyi.jpg Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hussein Ali Mwinyi
No image.svg Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Professor. Joyce Lazaro Ndalichako
Faili:Medard Kalemani.jpg Nishati Medard Matogolo Kalemani
No image.svg Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango
Augustine Mahiga (cropped).jpg Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dr. Augustine Philip Mahiga
No image.svg Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Ally Mwalimu
No image.svg Mambo ya Ndani Kangi Alphaxard Lugola
Charles Mwijage.jpg Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles John Mwijage
No image.svg Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe
William Lukuvi cropped.png Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
No image.svg Maliasili na Utalii Hamisi Andrea Kigwangalla
Makame Mbarawa IAEA.png Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa Mnyaa
No image.svg Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Aloyce Kamwelwe
(anahudhuria mikutano ya baraza la mawaziri bila kupiga kura
No image.svg Mwanasheria Mkuu wa Tanzania Dr. Adelardus Kilangi

MarejeoEdit

  1. Cabinet of Tanzania. tanzania.go.tz (May 2012). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-04-18. Iliwekwa mnamo May 2012.
  2. Katiba ya Tanzania, fungu 54. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-12-17. Iliwekwa mnamo 2015-12-11.
  3. Baraza la Mawaziri. Ikulu (10 December 2015). Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-12-22. Iliwekwa mnamo 2015-12-11.
  4. "Magufuli releases long awaited cabinet", 10 December 2015. 
  5. Chama Cha Mapinduzi [@ccm_tanzania] (10 December 2015). Rais Magufuli atangaza Baraza la Mawaziri (Swahili).

Tazama piaEdit

Wizara za Serikali ya Tanzania Orodha_ya_Mawaziri_Wakuu_wa_Tanzania