Barbato (Cerreto Sannita[1], Italia, 602- Benevento, 19 Februari 683) alikuwa askofu wa Benevento kwa miaka 19.

Kama padri alipinga kwa nguvu zote ushirikina na Upagani, na baada ya kufanywa askofu alipinga katika mitaguso mbalimbali fundisho la kwamba Yesu alikuwa na utashi wa Kimungu tu, si ule wa kibinadamu pia. Inasimuliwa kwamba aliwaongoa Walombardi na mtawala wao kwa Kristo.[2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Februari[3][4].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.