Barua za Shaaban Robert 1931-1958
Barua za Shaaban Robert 1931-1958 ni mkusanyo wa barua zipatazo kama mia moja ambazo zilihifadhiwa na Yusuph Ulenge kwa zaidi ya miaka sitini kabla ya kuja kukabidhiwa kwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili mnamo mwaka 1993 wakati wataalamu toka katika taasisi hiyo walipokuwa wakifanya utafiti. [1]
Kitabu hiki ni zawadi nzuri kwa waandishi na watunzi wa mashairi kwa sababu kimeelezea mambo ambayo yalikuwa hayafahamiki na wengi kuhusu Shaaban Robert na ukoo wake [2]
Katika kitabu hiki, kimedhihirisha pia uwezo mwingine wa Shaaban Robert wa kuzungumza na kuandika lugha ya kigeni ya Kiingereza, jambo ambalo wengi walikuwa hawafahamu kama mtaalamu huyo wa Kiswahili alikuwa anafahamu hadi lugha za kigeni na hata kusoma kwa njia ya posta.
Ndani ya kitabu hiki, msomaji ataweza kufahamu zaidi kuhusu imani aliyokuwa nayo Shaaban Robert katika suala la elimu hadi kumsisitizia ndugu yake Yusuoh Ulenge asimame katika elimu.
Tanbihi
hariri- ↑ Robert, Shaaban, 1909-1962. (2003). Barua za Shaaban Robert, 1931-1958. Mulokozi, M. M. (Mugyabuso M.), Ulenge, Yusuf, 1917-, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es Salaam, Tanzania: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. ISBN 9976-911-62-9. OCLC 54023065.
{{cite book}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ "University of Dar es Salaam - Institute of Kiswahili Studies". www.udsm.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2020-02-07.
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Barua za Shaaban Robert 1931-1958 kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |