Basiano wa Lodi

Basiano wa Lodi (kwa Kilatini: Bassianus; 310 hivi - Siracusa, Sicilia, Italia, 19 Januari 409) alikuwa askofu wa mji huo wa Italia Kaskazini kuanzia mwaka 373 hadi kifo chake.

Mt. Basiano.

Kama kijana aliyekwenda Roma kwa masomo, na huko aliongokea dini ya Ukristo. Baba yake alitaka aasi na kurudi nyumbani, lakini yeye alikataa na kukimbilia Ravenna.

Baada ya kuchaguliwa askofu, alishiriki mtaguso wa Akwileia (381) na labda hata mtaguso wa Milano (390). Alisaini pamoja na rafiki yake askofu Ambrosi wa Milano barua kwa Papa Sirisi.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Januari[1].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.