Batahaliye
Batahaliye alikuwa mke na dada wa mfalme wa Nubia Harsiotef (alitawala takriban mwaka 400 KK). Anajulikana kutoka kwenye stela ya mumewe na mazishi yake huko Nuri. Cheo chake kikuu kilikuwa mke mkubwa wa mfalme.[1] (sio mke mkuu wa mfalme kama kawaida). Vyeo vingine ni mke wa mfalme na dada wa mfalme.
Anajulikana pia kutokana na mazishi yake huko Nuri. Mazishi hayo yalikuwa ni piramidi yenye hekalu na vyumba viwili vya maziko chini ya ardhi. Kulikuwa na ngazi inayoingia chini ya ardhi na kuelekea kwenye vyumba viwili. Piramidi ilikutwa ikiwa imevunjwa, lakini vipande vya shabti visivyo na maandishi vilipatikana. Hapo pia ilipatikana stela inayoonyesha Batahaliye mbele ya miungu ya Ulimwengu wa chini Osiris,[2] Maelezo yake yalichorwa kwa hieroglifi za Misri, lakini maandishi yake ni magumu kusoma.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Batahaliye kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |