Mji wa Batman.

Batman (ni kifupi cha Milima ya Batı Raman) ni jina la mji mkuu wa Mkoa wa Batman, katika Uturuki. Mji huu pia unajulikana kwa jina la Êlih au Iluh kwa Kikurdi.[1] Ni mji ulioko katika Mto Batman ambao unajulikana sana kwa jina la Kikurdi mjini kusini-mashariki mwa nchi ya Uturuki.[2]

SerikaliEdit

Meya wa mji wa Batman ni Mh. Hüseyin Kalkan, ambaye ni mwanachama wa chama cha Democratic Society Party (DSP).

UchumiEdit

Mkoa wa Batman ni eneo muhimu kabisa la uzalishaji wa mafuta, na mji wa Batman una maeneo ya kale ya vifaa vya kale vya kuchimbia mfuta, ambavyo vilianzishwa tangu mwaka wa 1955.

Kuna takriban km 494 (na mi 307) ya bomba la kupitishia mafuta kutoka mjini Batman na kuelekea İskenderun. Kuna njia ya reli iliyokaribu kidogo na Kurtalan ambayo imeunganisha njia hiyo hadi kutoka katika mji wa Istanbul. Katika mji wa Batman, pia kuna uwanja wa ndege wa mkoa.

Histria ya mji na wakaziEdit

Hadi kufikia miaka ya 1950, mji wa Batman ulikuwa kama kaji-kijiji kidogo. Pale makampuni ya mafuta yalipoingia katika mji uchumi wa mji huo ukaanza kukua, na idadi ya makazi ya watu ikaanza kuongezeka.

Wafanyakazi wengi na maofisi mengi ya serikali yapo mjini. Kwa sasa idadi ya watu wasio na kazi katika mji huo inaanza kuonekana kuwa kubwa kuliko hapo awali.

Malezo na marejeoEdit

Viungo vya njeEdit