Beactant
Bericant, inayouzwa kwa jina la chapa Survanta, ni dawa inayotumika kuzuia na kutibu ugonjwa wa shida ya kupumua kwa watoto wachanga.[1] Hasa hutumiwa kwa wale waliozaliwa kabla ya wakati.[1] Dawa hii inatolewa kwenye koo.[1] Athari zake huanza ndani ya dakika chache na zinaweza kudumu kwa hadi siku tatu.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na mapigo ya moyo ya polepole, oksijeni kidogo, shinikizo la chini la damu, shinikizo la juu la damu, kukosa pumzi (apnea), na kuziba kwa mrija wa ndani ya koromeo (endotracheal tube).[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha hali hatari ya kingamwili kupigana na tsishu na viungo vyake (sepsis).[1] Dawa hii ni surfactant ya mapafu inayotokana na ng'ombe.[1]
Beractant iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1991.[1] Nchini Marekani, miligramu 100 hugharimu takriban dola 400 za Marekani kufikia mwaka wa 2022.[2]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "Beractant Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Survanta Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Beactant kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |