Beatrix Mugishagwe
Beatrix Mugishagwe ni mwongozaji filamu Mtanzania. Ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya filamu ya Abantu Visions, pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa taasisi ya Tanzania Independent Producers Association(TAIPA). [1]
Maisha yake
haririMugishagwe alisomea utengenezaji filamu Ujerumani Magharibi,Alifanya kazi kwenye televisheni kwa miongo miwili huko Ujerumani kabla ya kurudi Tanzania mnamo mwaka 1994. [1]
Alianzisha kampuni yake ya uzalishaji filamu Abantu Visions, na kuandaa makala ya Kiswahili ya mazingira yenye sehemu ishirini na nne pamoja na makala nyingine iliyohusu viongozi wa kike wa Afrika iliyowasilishwa na Bi.Angélique Kidjo. Makala hii ilihusu wanawake kama Ellen Johnson Sirleaf, Graça Machel na Wangari Maathai[1] pamoja na Imruh Bakari na mhadhiri Augustine Hatar. [1]
Bi. Mugishagwe alihusika katika utengenezaji wa filamu ya Tumaini (2005). Kupitia filamu hii alipokea kiasi cha $400,000 kutoka ubalozi wa Norway pia Alipokea tuzo ya Unicef na tuzo ya SIGNIS.[1]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 Bryce, Jane (2010). "Outside the Machine? Donor Values and the Case of Film in Tanzania". Katika Mahir Saul; Ralph A. Austen (mhr.). Viewing African Cinema in the Twenty-First Century: Art Films and the Nollywood Video Revolution. Ohio University Press. ku. 165–72. ISBN 978-0-8214-1931-1.
{{cite book}}
: CS1 maint: multiple names: editors list (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Beatrix Mugishagwe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |