Bendera ya Eswatini
Bendera ya Eswatini ina milia ya rangi za buluu, njano na nyekundu. Katikati iko ngao ya kijeshi ya Kiafrika yenye rangi nyeusi na nyeupe pamoja na mikuki ya njano.
Upana wa milia ni katika uhusiano wa 3:1:8:1:3. Rangi zina maana ifuatayo:
- Nyekundu hukumusha damu iliyomwagika katika vita za nyakati zilizopita
- Njano hudokeza utajiri wa madini ya nchi
- Buluu iwee rangi ya amani
Ngao ni ile ya kikosi cha jeshi cha Emasotsha inayopatikana pia ndani ya nembo ya nchi. Rangi za ngao zinasomwa kukumbusha ya kwamba watu weusi na weupe huishi pamoja kwa amani.
Bendera hii ilianzishwa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kama alama ya kikosi cha Waswazi waliopigania vita upande wa Uingereza.