Bendera ya Zambia
Bendera ya Zambia ni ya kijani. Katika kona ya chini kuna eneo ndogo la milia mitatu ya kusimama ya nyekundu, nyeusi na dhahabu. Juu yake iko tai ya dhahabu.
Bendera hii imetokana na bendera ya chama cha kupigania uhuru United National Independence Party (UNIP). Imechukuliwwa kama bendera rasmi ya taifa wakati wa uhuru 24. 10. 1964. Ilibadilishwa kidogo mwaka 1996.
Rangi ni zilezile za Ethiopia au rangi za Umoja wa Afrika pamoja na rangi nyeusi.
Rangi zinaelezwa mara nyingi kwa njia ifuatayo:
- Kijani ni ya mashamba na misitu
- Dhahabu ni ya utajiri wa madini hasa shaba
- Nyeusi ni rangi ya watu
- nyekundu ni ya mapambano ya kupigania uhuru
Tai ni ndege ya mto Zambezi iliotoa jina lake kwa nchi ya Zambia.