Bernard Agré
Kadinali wa Ivory Coast
Bernard Agré (2 Machi 1926 – 9 Juni 2014) alikuwa Askofu Mkuu wa Abidjan, Côte d'Ivoire, na kardinali wa Kanisa Katoliki.[1]
Wasifu
haririAlizaliwa Monga, Côte d'Ivoire[2]. Alisoma katika Seminari ya Bingerville ambako alisomea falsafa, kisha akaendelea katika Seminari Kuu ya Quidah, Dahomey (sasa Benin), ambako alisomea theolojia. Hatimaye, kati ya mwaka 1957 hadi 1960, alisoma katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana huko Roma, ambako alipata shahada ya uzamivu (PhD) katika theolojia kwa heshima ya juu zaidi, summa cum laude.
Marejeo
hariri- ↑ "Biographical Dictionary of John Paul II (1978-2005), Consistory of February 21, 2001 (VIII)". Florida International University website, The Cardinals of the Holy Roman Church section.
- ↑ Catholic News Agency website, Agre, Bernard
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |