Besifloxacin
Besifloxacin, inayouzwa kwa jina la chapa Besivance, ni dawa ya kukinga inayotumika kutibu mwasho wa utando wa nje wa mboni ya jicho na kope la ndani utokanao na bakteria.[1] Inatumika kama tone la jicho.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na uwekundu wa jicho.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio.[2] Usalama wake katika ujauzito hauko wazi.[2] Ni fluoroquinolone na hufanya kazi kwa kuzuia DNA topoisomerases.[2]
Besifloxacin iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya matibabu nchini Marekani mwaka wa 2009.[1] Nchini Marekani, chupa ya mililita tano inagharimu takriban dola 210 kufikia mwaka wa 2022.[3]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "DailyMed - BESIVANCE- besifloxacin suspension". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 "Besifloxacin Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Besivance Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)