Betriksabani
Betriksabani (Betrixaban), iliyouzwa kwa jina la chapa Bevyxxa miongoni mwa mengine, ilikuwa dawa iliyotumika kuzuia kuganda kwa damu kwenye mishipa ya watu wazima walio hatarini, waliolazwa hospitalini kwa ugonjwa.[1] Ina kiwango cha juu cha kutokwa na damu ikilinganishwa na enoxaparin.[2] Dawa hii ilichukuliwa kwa mdomo.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kutokwa na damu.[3] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio.[3] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[3] Ni kizuizi cha moja kwa moja cha Xa.[3]
Betriksabani iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2017; hata hivyo, ilisitishwa baadaye.[3] Ilikataliwa kuidhinishwa barani Ulaya mnamo mwaka wa 2018 kwa sababu ya wasiwasi kuhusu ufanisi na usalama wake.[2]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 Research, Center for Drug Evaluation and. "Approved Drugs - FDA approved betrixaban (BEVYXXA, Portola) for the prophylaxis of venous thromboembolism (VTE) in adult patients". www.fda.gov (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-25. Iliwekwa mnamo 2018-10-29.
- ↑ 2.0 2.1 "Dexxience". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 "Betrixaban Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Betriksabani kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |