Bettina Mary Arndt (amezaliwa Agosti 1 1949) ni mwandishi kutoka Australia na ni mchangiaji aliyejikita kuzungumzia masuala ya kujamiiana na jinsia. Alianza kama mtaalamu na mtetezi wa masuala ya kike, alikuja kupata umaarufu mwaka wa 1970, alianza kazi ya utangazaji na uandishi na aliweza kuandika vitabu kadhaa. Ndani ya miongo miwili iliyopita aliachana na masuala ya kutetea haki za wanawake na kujikita kuzungumzia masuala ya manyanyaso ya kijinsia na masuala ya ukatili pamoja na kutetea haki za wanaume.

Bettina Arndt

Maisha

hariri

Arndt alizaliwa katika mji wa Penrith, Uingereza. Baba yake alikuwa Heinz Arndt (1915-2002) na mama yake Ruth (nee Strohsahl) (20 March 1915 - 20 March 2001). Ni mtoto wa mwisho kati ya watoto watatu. Wazazi wake walikuwa Wajerumani walioukimbia utawala wa kinazi wa Ujerumani. Walihamia Australia mwaka 1945.

Mwaka 1971 baada ya kumaliza Shahada ya Sayansi katika Chuo cha Taifa cha Australia , alihamia Sydney na alijiunga na chuo cha New South Wales na alitunukiwa shahada ya uzamili katika masuala ya saikolojia mwaka 1973; tafiti zake zilihusu matatizo ya ufikaji wa kileleni.

Familia

hariri

Arndt anaishi Woollahra pembezoni mwa mji wa Sydney New South Wales. Aliolewa mara ya kwanza na mwanahabari Dennis Minogue aliyefariki mwaka wa 1981. Arndt na Minogue walikuwa wanafanya biashara pamoja. Aliolewa mara ya pili na wakili wa Marekani Warren Scott mwaka 1986. Walifunga ndoa yao Watson's Bay, Sydney, na walitalakiana mwaka 2007. Kati ya mwaka 1986 hadi 1991 aliishi na Scott katika mtaa wa Manhattan jijini New York City NY. Arndt watoto wawili wa kiume na mmoja wa kike.

Baada ya kuhitimu, Arndt alikuwa kati ya watu wachache waliyofanya kazi ya utaalamu wa kujamiana mapema mwaka 1970. Alihudumia kliniki katika mji wa Sydney hasa wanawake.

Arndt alijulikana zaidi miaka sabini baada ya kuwa mhariri wa Forum, gazeti lililokuwa likizungumzia masuala ya kujamiana, kilichopelekea kuonekana kwake mara kadhaa katika vipindi vya televisheni. Aliteuliwa kama mhariri mwaka wa 1974 na alihudumu katika nafasi hiyo hadi Julai 1982. Katika kipindi hicho cha kazi yake alionekana katika vipindi vya televisheni kama mfululizo wa kipindi cha Muda wa maisha yangu mwaka (2013). Makala hayo yamesababisha matatizo katika bunge la QueensLand na mbunge Des Frawley alitoa tamko kuwa ni gazeti chafu na polisi walivanmia ofisi na kuchukua nakala za gazeti hilo, kati ya 1973 na 1976 bodi ya kurusha matangazo ya australia iliamuru kuwa televisheni na radio zote zilizokuwa zinarusha vipindi vya Arndt virekodi vipindi hivyo kwanza kabla ya kuvirusha ili viweze kuhakikiwa na uongozi.Bodi ilitoa sababu ya kwanini inawekea vikwazo kwa vipindi vyake ambavyo vilikuwa vikionyeshwa muda ambao familia zinatazama televisheni na wazazi walikuwa wanataka kudhibiti maudhui ya ngono yasiwafikie watoto wao.

Mwaka 1978 aliafanya mapinduzi kuhusiana na maswala ya kujamiana ili kuangalia ni kwa kiasi gani watu wanaelewa maswala ya ngono na mitazamo yao kuhusu ngono.Alitambua kuwa harakati za wanawake zilileta maswala ya kujitambua katika maswala ya kujamiana, na kuna umuhimu wa kujamiana kwa watu wazima na watu wasiojiweza na aliwapa sifa viongozi wa kusuni mwa Australia kwa kuweka sheria ya ubakaji kwenye ndoa. Kazi yake ya elimu ya kujamiana ilihusisha wasomi wa ngazi tofauti ikiwemo madaktari na wataalamu wengine.Baada ya kifo cha aliyakuwa mume wake na mfanyabiashara mwenzie,Dennis Minogue, mwaka 1981,gazeti la 'Forum' lilifungwa.Katika miaka ya 1980,Arndt alifanya kazi kama mwandishi kwenye gazeti la playboy na aliandika kuhusiana na maswala tofauti ya kijamii kwenye magazeti ya 'The Sydney Morning Herald ' na 'The Age'.Kwenye kipindi hiki Arndt alimiliki kipindi chake cha radio.Mwaka 1982 alionekana kipindi cha televisheni ambacho ni mfululizo wa 'Beauty and the beast' na kuanzia kipindi cha kuanzia 1981 hadi 1986 alitokea katika kipindi cha 'Today Show'. Mwaka 1983 gazeti la 'The Sydney Morning Herald' lilimtaja Arndt kama mwanaharakati jasiri kwenye maswala ya kujamiana. Mwaka 1984 Arndt alianzisha biashara ya nguo za ndani na vifaa vya bandia vya ngono, aliandika vitabu vya kufundisha maswala ya kujamiana na vitabu vingine. Mwaka 1986 alihamia New York City kwa miaka mitano , alipokuwa anishi Marekani aliandika kila wiki makala ya gazeti kupitia 'The Age Melbourne'.Alianidika vitabu na baadaye alirudi Australia.


Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bettina Arndt kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.