Bezlotoxumab, inayouzwa kwa jina la chapa Zinplava, ni dawa inayotumika katika maambukizo ya <i id="mwDQ">Clostridium difficile</i> ili kuzuia kutokea kwake tena.[1] Dawa hii inatumika pamoja na antibiotiki[1] na inatolewa kwa njia ya sindano kwenye mshipa.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, kuhara, homa na maumivu ya kichwa.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kushindwa kwa moyo.[2] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[3] Dawa hii ni kingamwili ya monokloni inayojifungamanisha na sumu ya Clostridia difficile B.[2]

Bezlotoxumab iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2016 na Ulaya mwaka wa 2017.[2][1] Nchini Uingereza, kichupa cha miligramu 1,000 hugharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £2,500 kufikia mwaka wa 2021.[4] Kiasi hiki nchini Marekani kinagharimu takriban dola 4,000 za Marekani.[5]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Zinplava". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 "DailyMed - ZINPLAVA- bezlotoxumab injection, solution". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Bezlotoxumab (Zinplava) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Desemba 2020. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1338. ISBN 978-0857114105.
  5. "Zinplava Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bezlotoxumab kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.