Bisibisi
Bisibisi ni kifaa cha ufundi kinachotumiwa kugeuza skurubu (parafujo) yenye kofia iliyo na tundu ama kwa kuikaza au kuifungua..
Bisibisi huwa na shikamano upande moja inayowezesha mkono kuishika vizuri. Mwisho wake una umbo unaolingana na umbo la tundu kwenye kofia ya parafujo.
Maumbo ya kawaida ni ama tundu nyoofu au tundu msalaba. Kuna aina mengine kwa maumbo mbalimbali ya kofia za parafujo za pekee.