Bivalirudini (Bivalirudin), inayouzwa kwa majina ya chapa Angiomax na Angiox, ni dawa inayotumiwa wakati wa utaratibu wa kufungua mishipa ya moyo iliyoziba ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu kwenye moyo (percutaneous coronary intervention).[1] Inaweza kutumika kwa watu walio na hali ambapo matumizi ya heparini husababisha kupungua chembechembe za damu za pletleti (heparin-induced thrombocytopenia)[1] na inatolewa kwa njia ya kudungwa sindano kwenye mshipa.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kutokwa na damu.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[1] Dawa hii ni kizuizi cha cha moja kwa moja cha thrombin (kimeng'enya kinachosaidia damu kuganda) na ni toleo la viwandani la hirudin (ambayo pia huzuia utendakazi wa thrombin).[1][2]

Bivalirudini iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2000.[1] Ingawa iliidhinishwa barani Ulaya mnamo mwaka wa 2004, idhini hii iliondolewa.[3] Inapatikana kama dawa ya kawaida.[2] Nchini Marekani, miligramu 250 hugharimu takriban dola 115 za Kimerekani kufikia mwaka wa 2022.[4]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "DailyMed - BIVALIRUDIN injection". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "Bivalirudin Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 11 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Angiox". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 10 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Bivalirudin Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 11 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bivalirudini kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.