Black Panther (filamu)
Black Panther ni filamu ya Marekani ya 2018 inayotokana na mhusika wa Marvel Comics. Filamu hii imetolewa na Marvel Studios na kusambazwa na Walt Disney Studios Motion Picture', ni filamu ya kumi na nane kutoka kampuni ya marvel Cinematic Universe (MCU). Filamu hii iliongozwa na Ryan Coogler, ambaye aliaandika akishirikiana na Joe Robert Cole. Nyota wa filamu hii ni pamoja na Chadwick Boseman kama T'Challa / Black Panther, pamoja na Michael B. Jordan, Lupita Nyong'o, Danai Gurira, [[Martin Freeman, Daniel Kaluuya]], Letitia Wright, Winston Duke, Angela Bassett, Forest Whitaker, na Andy Serkis. Kwenye filamu hii, T'Challa ni mfalme wa Wakanda baada ya kifo cha baba yake, lakini ufalme wake unawekwa hatarini na adui yake ambaye ana mpango wa kuachana na sera za nchi hiyo za kujitenga na kuanzisha mapinduzi ya kimataifa.
Wesley Snipes alikuwa na nia ya kuitoa filamu ya Black Panther mwaka wa 1992, lakini mradi huu haukufanikiwa. Mnamo Septemba 2005, Marvel Studios ilitangaza filamu ya Black Panther kama moja ya kati ya filamu kumi zinazotokana na wahusika wa Marvel Comics na kusambazwa na Paramount Pictures.
External links
haririMakala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |