Blogu ni teknolojia mpya inayowezesha watu binafsi kuchapa maoni na fikra zao katika mtandao wa tarakilishi maarufu kama wavuti au intaneti. Blogu inaweza kuchukuliwa kama ni shajara pepe.

Uandishi wa Blogu
Uandishi wa Blogu

Neno la Kiswahili "blogu" linatokana na neno la Kiingereza, "blog", ambalo limetokana na neno lingine, "weblog".

Kimsingi, blogu ni aina ya tovuti ambayo huandikwa mara kwa mara na kwa mpangilio wa mambo mapya kutokea ukurasa wa mbele kuendana na tarehe na mwezi.

Aina za blogu

hariri

Katika blogu za binafsi, waandishi hutoa mawazo yao kuhusu masuala ibuka katika jamii na kwa njia hii kuanzia mazungumzo katika intaneti. Wasomaji wanaweza kuchangia na kuendeleza katika mawazo haya kwa kupeana maoni yao yanayoweza kukubaliana na yale ya mwenye blogu au hata kutofautiana. Mawazo haya ya wasomaji huwekwa kwa komenti ambazo huwa pale chini ya blogu.

Wanablogu wanaweza kuchochea hisia nzito katika jamii kama zile za uanaharakati au siasa.

Ili kuwa na blogu yako binafsi, wafaa kuwa unajua kutumia intaneti na pia uwe na jambo la kuwafahamisha watu au kuwafunza ili upate wasomaji. Wafaa pia uwe na mtindo.

Blogu za kampuni huwa na lengo maalumu ya kuwafahamisha wasomaji kuhusu bidhaa mbali mbali za kampuni. Wenye kampuni huzitumia pia kuwafahamisha wateja na wasomaji kuhusu mambo mapya katika kampuni.

Zipo blogu za aina mbalimbali. Kwa mfano, blogu za maandishi, blogu za mkononi, blogu za picha, blogu za sauti, na blogu za video.

Blogu ya mradi wa Global Voices inaandika muhtasari wa majadiliano na habari zinazojitokeza katika blogu mbalimbali duniani, hasa nje ya Marekani. Mradi huu una wanablogu katika nchi mbalimbali duniani ambao wanaandika juu ya masuala muhimu yanayojitokeza katika blogu za nchini mwao au katika bara lao.

Blogu za sauti

hariri

Tofauti na blogu za maandishi ambapo mwenye blogu huwa na mtindo wa kuandikaandika katika shajara hiyo yake, blogu za sauti huwa na sauti za mwenyewe akiongea au akihoji watu. Wanaomfuata huja na kusikiza sauti zile.

Blogu za video au vlogu

hariri

Kando na blogu ambayo huwa na maandishi na picha pekee, pia kuna vlogu ambayo huwa na video. Mwenye vlogu huchukua video akifanya mambo kama mafunzo, kuoka mikate, kupika, kutengeneza simu na watu hufuata vlogu yake ili waweze kusoma.Unapokuwa na blogu ya aina hii, lazima uwe na kamera nzuri ya kuchukua video zako na pia uwe na uwezo wa kurekebisha video.

Viungo vya nje

hariri