Bromfenac ni dawa isiyo ya steroidi (homoni) ya kupunguza maumivu na kuvimba (nonsteroidal anti-inflammatory drug) ambayo hutumiwa kutibu maumivu na uvimbe baada ya upasuaji wa kuondoa ukungu kwenye lenzi ya jicho (cataract surgery).[1] Dawa hii inatumika kama tone la jicho mara mbili kwa siku kwa muda wa wiki mbili.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na macho mekundu, kuwasha macho na maumivu ya kichwa.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha uponyaji wa polepole wa jeraha, kutokwa na damu na keratiti, yaani kuvimba kwa utando wa nje wa jicho (keratitis).[1] Dawa hii inafanya kazi kwa kuzuia uzalishaji wa prostaglandini (kemikali zinazozalishwa mwilini na zinazotumika katika kudhibiti uvimbe, maumivu na utendaji wa viungo kama vile tumbo, figo na mfumo wa uzazi).[1]

Bromfenac iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2005.[1] Dawa hii inapatikana kama dawa ya kawaida.[2] Nchini Marekani mililita 1.7 ya myeyusho wa 0.09% inagharimu takriban dola 51 kufikia mwaka wa 2021.[2] Nchini Uingereza mililita 5 ya myeyusho wake hugharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa pauni 8.5.[3]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Bromfenac Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 17 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "Bromfenac Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Mei 2020. Iliwekwa mnamo 17 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. BNF (tol. la 80). BMJ Group and the Pharmaceutical Press. Septemba 2020 – Machi 2021. uk. 1241. ISBN 978-0-85711-369-6.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: date format (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bromfenac kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.