Buingamia
Buingamia (Solpugidae: Zeria loveridgei)
Buingamia (Solpugidae: Zeria loveridgei)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropodi (Wanyama bila uti wa mgongo wenye mwili wa vipingili na miguu yenye viungo)
Nusufaila: Chelicerata (Arthropodi wenye mwili wa mapande mawili na maungo mawili mbele ya domo)
Ngeli: Arachnida (Arthropodi wenye miguu minane)
Nusungeli: Dromopoda
Oda: Solifugae (Wanyama kama buingamia)
Sundevall, 1833
Ngazi za chini

Familia 12:

Buingamia ni arthropodi wa oda Solifugae katika ngeli Arachnida. Mara nyingi watu huchanganya buingamia na nge au buibui wakubwa lakini sio wale wa kwanza wala wa pili. Wote wamo katika oda yao ya kibinafsi, nge katika Scorpiones na buibui katika Araneae.

Tofauti dhahiri zaidi kati ya buingamia na nge ni ukosefu wao wa mkia wenye msumari wa sumu kwa ncha yake. Pia hawana magando kwenye pedipalpi zao. Tofauti kuu na buibui ni kutokuwepo kwa chuchu za kukalidi hariri, kwa hivyo hawawezi kutengeneza utando. Na kinyume na buibui wanapumua kupitia mfumo wa spirakulo na trakea ulioundwa vizuri badala ya kwa njia ya mapafu-kitabu.

Spishi za Afrika ya Mashariki hariri

  • Biton brunnipes Pocock, 1896
  • Biton tigrinus Pocock, 1896
  • Biton velox Simon, 1885
  • Bitonupa kraepelini Roewer, 1933
  • Blossia massaica Roewer, 1933
  • Blossia obsti (Roewer, 1933)
  • Blossia sulcichelis (Roewer, 1941)
  • Blossia toschii (Caporiacco, 1949)
  • Ceroma hessei Roewer, 1933
  • Ceroma macrognatha Lawrence, 1954
  • Ceroma ornatum Karsch, 1885
  • Ceroma similis Roewer, 1941
  • Galeodes arabs Koch, 1842
  • Hemiblossia bouvieri Kraepelin, 1899
  • Hemiblossia brunnea Lawrence, 1953
  • Rhagodes karschi Kraepelin, 1899
  • Rhagodes massaicus Roewer, 1933
  • Rhagodoca baringona Roewer, 1933
  • Rhagodoca bettoni Roewer, 1933
  • Rhagodoca immaculata Roewer, 1933
  • Rhagodoca ornata (Pocock, 1895)
  • Rhagodoca phillipsii (Pocock, 1896)
  • Rhagodoca smithii (Pocock, 1897)
  • Rhagodoca termes (Karsch, 1885)
  • Solpuga roeweri Fage, 1936
  • Solpugiba svatoshi (Birula, 1926)
  • Solpugisticella kenyae Turk, 1960
  • Solpugyla centralis (Hewitt, 1927)
  • Solpugyla kigoma Roewer, 1961
  • Solpugyla masienensis (Lawrence, 1929)
  • Tarabulida mugambii Kristie Reddick, Charles M. Warui Robert Wharton, 2010
  • Zeria albistriata (Roewer, 1933)
  • Zeria atra (Roewer, 1933)
  • Zeria atrisoma (Roewer, 1933)
  • Zeria capitulata (Karsch, 1885)
  • Zeria fordi (Hirst, 1907)
  • Zeria greta (Roewer, 1933)
  • Zeria lobatula (Roewer, 1933)
  • Zeria loveridgei (Hewitt, 1925)
  • Zeria merope (Simon, 1879)
  • Zeria meruensis (Tullgren, 1907)
  • Zeria nasuta (Karsch, 1880)
  • Zeria niassa (Karsch, 1880)
  • Zeria nigrescens (Pocock, 1895)
  • Zeria obscura (Kraepelin, 1899)
  • Zeria sericea (Pocock, 1897)
  • Zeria sulfuripilosa (Roewer, 1933)
  • Zeria wabonica (Roewer, 1933)
  • Zeria zebrina (Pocock, 1898)
  • Zeriassa bicolor (Pocock, 1897)
  • Zeriassa inflexa Lawrence, 1953
  • Zeriassa intermedia Lawrence, 1953
  • Zeriassa lepida Kraepelin, 1914
  • Zeriassa ruspolli (Pavesi, 1897)
  • Zeriassa spinulosa Pocock, 1898
  • Zeriassa wabonica Roewer, 1933

Picha hariri

  Makala hii kuhusu "Buingamia" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili camel spider kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni buingamia.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Buingamia kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.