Buni ni kituo cha teknolojia kinachosaidia watu (hasa vijana) kuhusiana na mambo ya ugunduzi na ujasiriamali wa kiteknolojia kwa kuwajengea watu uwezo, kuwashauri watu na uwezeshaji wa jamii nzima kwa ujumla juu ya mambo yahusuyo teknolojia.Buni ilianzishwa mnamo mwaka 2011 ndani ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)[1] nchini Tanzania .[2]

Dhamira ya Buni hariri

Dhamira kuu ya Buni ni kugundua, kulea na kushauri vijana kuhusiana na ugunduzi wa njia za kiteknolojia zinazoweza kutatua matatizo mbalimbali nchini Tanzania.

Marejeo hariri

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-05-20. Iliwekwa mnamo 2021-05-30. 
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-29. Iliwekwa mnamo 2017-08-19.