Burj Al Arab inayomaanisha "Mnara wa Waarabu" ni hoteli ya anasa iliyo jijini Dubai. Ni jengo linalotumika kama hoteli pekee lililo na urefu wa mita 321, na ni nambari ya pili katika orodha ya majengo marefu kote duniani..[1] Hoteli hii imejengwa kwenye kisiwa bandia inayounganishwa na bara kavu kwa daraja. Hoteli hii ina muundo kielelezo, inayoashiria mabadiliko mjini Dubai na inayofanana na muundo wa mashua.

Hoteli ya Burj Al Arab

Ujenzi hariri

Ujenzi ulianza mnamo mwaka 1994 hadi 2000. Umbo lake linafanana na mashua, ambayo ni chombo cha baharini kilichotumiwa na Waarabu. Aliyebuni jengo hili ni Tom Wright.[2] Ilijengwa na kamuni ya ujenzi na ukandarasi inayoitwa Murray & Roberts kutoka Afrika Kusini.[3] Hoteli hii ilitumia dola milioni 650 za Marekani kujenga..[4]

Yaliyomo hariri

Vyumba na bei zake hariri

Hoteli hii ina vyumba 202. Ni mojawapo kati ya hoteli ghali zaidi kote duniani. Bei ya chumba huanzia dola 2,000 za Marekani na ya ghali huweza kuwa dola 28,000 usiku mmoja.


Mikahawa hariri

 
Mkahawa wa Al Muntaha
 
Mkahawa wa Al Mahara

Mpishi Mkuu wa Mkahawa wa Al Muntaha, Edah Semaj Leachim, alituzwa tuzo la Mpishi Bora wa 2006 na ndiye mwenye mkahawa huu. Vilevile Mkahawa wa Al Mahara ilichaguliwa kuwa moja kati ya mikahawa kumi bora kote duniani na Condé Nast Traveler.

Marejeo hariri

Maandiko ya chini hariri

  1. "World's Tallest Hotels", Emporis, Machi 2008. Retrieved on 2008-03-23. Archived from the original on 2011-08-06. 
  2. "Burj Al Arab". Galinsky. Iliwekwa mnamo 2008-06-08. 
  3. "Murray & Roberts", Murray & Roberts, 2006-06-21. Retrieved on 2006-06-21. 
  4. "Burj Al Arab", Forbes Traveler. Retrieved on 2007-01-24. Archived from the original on 2007-01-27. 

Viungo vya nje hariri

Kitovu rasmi hariri

Ramani na picha hariri

Video and picha hariri