Buzz Aldrin
Dr. Edwin Eugene "Buzz" Aldrin, Jr. (*20 Januari 1930) ni rubani na mwanaanga kutoka nchi ya Marekani. Alikuwa mtu wa pili kukanyaga uso wa Mwezi alipofika pamoja na Neil Armstrong kwenye safari ya chombo cha anga cha Apollo 11.
Aldrin na Armstrong walifika mwezini tarehe 20 Julai 1969 wakiwa watu wa kwanza waliomaliza safari hadi gimba la angani tofauti na Dunia yetu.[1]
Aldrin aliwahi kusoma uhandisi mitambo kwenye chuo cha kijeshi cha West Point mnamo 1951. Aliendelea hadi kupokea shahada ya uzamivu ("PhD") katika fani ya usafiri wa angani kwenye Chuo cha Massachusetts Institute of Technology (MIT) mnamo 1963.
Aliteuliwa kwa safari ya kwenda mwezini na kufika pale alipokuwa na umri wa miaka 39.
Maisha ya baadaye
haririAldrin aliondoka katika utumishi wa NASA mnamo 1972 akaendelea katika jeshi la anga. Alikuwa na matatizo ya kuozea maisha ya kawaida akipambana kwa miaka kadhaa na majonzi na ulevi.
Baada ya kustaafu kabisa alitunga vitabu kadhaa kuhusu maisha yake.
Aldrin alioa mara tatu akipata na watoto watatu kutoka ndoa yake ya kwanza.
Marejeo
hariri- ↑ Buzz Aldrin, Ken Abraham: (2009) "Magnificent Desolation", Random House Publishers, p. 26