By The Tree
By The Tree ni kundi la muziki wa Kikristo la kisasa lililoshinda tuzo ya Dove mara mbili.
By The Tree | |
---|---|
By The Tree wakiwa wameshinda tuzo za Dove.
| |
Maelezo ya awali | |
Asili yake | Weatherford, Texas |
Aina ya muziki | Kikristo Nyimbo za Kikristo za Kisasa |
Kazi yake | Wanamuziki |
Miaka ya kazi | 1997 hadi sasa |
Studio | Fervent Records |
Wanachama wa sasa | |
Aaron Blanton Ben Davis Dustin Sauder Eric Green |
Historia
haririBy The Tree ilianzishwa katika Weatherford, Texas katika mwaka wa 1997 na Chuck Dennie na Bala Boyd.
Kama makundi mengi ya muziki, By The Tree walipata kuanza kazi yao kwa kuimba katika matukio madogomadogo - hasa katika makanisa - kote kusini na kusini magharibi wa Marekani. Kusafiri kwao na kufanya ziara mbalimbali kulikuza umati za mashabiki.
Katika mwaka wa 1999,walitoa albamu mbili za kujitegemea(bila kuwa na udhamini wa studio yoyote) ,wakarekodi wenyewe na wakaziuza katika matamasha yao na matukio waliohudhuria. Ilipofika mwaka wa 2001, 30,000 za albamu hizi zilikuwa zimeuzwa.Hii ilileta faida kubwa zaidi ya hela walizotumia kurekodi nyimbo hizo.Aidha ya hayo, iliwafanya wajulikane katika sekta ya nyimbo za Kikristo.
Hatimaye,bendi ilitia saini mkataba na Fervent Records, sehemu ya kampuni ya muziki ya BMG.. Albamu yao ya kwanza iliyorekodiwa ya kitaifa ilikuwa Invade My Soul. Albamu hii ilikuwa katika chati ya nyimbo bora 40 ya Billboard katika sehemu za nyimbo za kisasa na vile vile sehemu ya huru au kujitegemea. Albamu hii ilishinda tuzo mbili za Dove.Albamu yenyewe ikishinda tuzo ya Albamu Bora katika aina ya muziki ya Rock/Alternative na wimbo wa albamu ukishinda tuzo ya Nyimbo Bora Uliorekodiwa.
Bendi hili limebadilika mara kadhaa tangu kutia saini mkataba na Fervent huku wanachama wengine wakiongezeka na wengine kutolewa. Mwimbaji na mchezaji gitaa ,Aaron Blanton aliungana na kundi hilo kabla ya kurekodi kwa Invade My Soul na Samuel McKern(mchezaji ngoma) akiondoka. Chuck Dennie alikuwa mwimbaji kiongozi na mchezaji gitaa hadi mwaka wa 2005. Ben Davis alijiunga nao katika mwaka wa 2002 kwa ajili ya kurekodi These Days. Mwanachama wa hapo awali wakianza,Kevin Rhoads,aliondoka muda mfupi kabla ya kutolewa kwa These Days na nafasi yake kuchukuliwa na Charlie Goddard (aliyeondoka bendi katika mwaka wa 2003 kuungana na bendi la Jeff Deyo).
By The Tree imetoa albamu nne likiwa na Fervent Records na wao ni kundi maarufu katika muziki ya Kikristo ya kisasa.
Chuck Dennie sasa anaishi Edmond,OK na mke wake Joanne na ni mfanyikazi katika kanisa lenye kampasi mbalimbali linalojulikana kama LifeChurch.tv kama mchungaji wa kuabudu katika kampasi ya Kaskazini Magharibi wa OKC.
Wanachama wa sasa
hariri- Aaron Blanton (mwimbaji/mchezaji gitaa)
- Ben Davis (piano/mwimbaji)
- Dustin Sauder (kiongozi wa kucheza gitaa/mwimbaji)
- Eric Green (mchezaji ngoma)
Wanachama wa zamani
hariri- Cameron Tucker – (Alishiriki katika "Passion For Jesus '99" na "Shoot Me Down")
- David Canington – piano (Alishiriki "Passion For Jesus '99" na "Shoot Me Down")
- Betsy Caswell –mwimbaji(Alishiriki "Passion For Jesus '99" na "Shoot Me Down")
- Kevin Rhoads – mwimbaji, mchezaji gitaa
- Samuel McKern – mchezaji ngoma
- Charlie Goddard – mwimbaji,mchezaji gitaa
- Rocky Presley –
- Chuck Dennie – mwimbaji,mchezaji gitaa
- Garrett Goodwin – mchezaji ngoma
- Dan Castillo – mchezaji gitaa ya bass
- James Putnam – mchezaji gitaa ya bass
- Melissa Stein – mwimbaji
Diskografia
hariri- Passion For Jesus (1999) Walirekodi na kusambaza wenyewe
- Shoot Me Down (1999) Walirekodi nakusambaza wenyewe
- Invade My Soul (Fervent Records, 2001) Nambari katika chati ya Marekani ya Kikristo #35
- These Days (Fervent, 2002) Nambari katika chati ya Marekani ya Kikristo #17
- Root (Fervent, 2003) Nambari katika chati ya Marekani ya Kikristo #15
- Hold You High (Fervent, 2004)
- World On Fire (Fervent, 2006)
- Beautiful One: The Best of By The Tree (Fervent, 2007)
Marejeo
haririViungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu By The Tree kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |