Can't Put It in the Hands of Fate

Mashairi yanazungumzia ubaguzi wa rangi

"Can't put It in the Hands of Fate" ni wimbo wa mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa Marekani Stevie Wonder, akiwashirikisha wanamuziki wanaorap ambao ni Rapsody, Chika, Cordae na Busta Rhymes. Ilizinduliwa tarehe 13 Oktoba 2020, ni wimbo wa kufurahisha wenye mashairi yanayozungumzia ubaguzi wa rangi wa kitaasisi, na masuala yanayohusiana kama vile ukatili wa polisi na vuguvugu la "Black Lives Matter"[1] ikiwa na maana kwamba Maisha ya Weusi ni muhimu.

Marejeo hariri

  1. "Stevie Wonder rejects 'all lives matter' in first new music in four years". the Guardian (kwa Kiingereza). 2020-10-13. Iliwekwa mnamo 2022-04-16.