Carbinoxamine, inayouzwa kwa jina la chapa Arbinoxa miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumika kutibu athari za mzio ikiwa ni pamoja na homa ya hay, kuvimba kwa mboni ya jicho kunakosababishwa na mzio, na mabaka mekundu yenye mwasho kwenye ngozi.[1] Dwa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1] Haipaswi kutumiwa kwa homa ya kawaida au kwa watoto chini ya miaka miwili.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhisi usingizi, kizunguzungu, uratibu mbaya na maumivu ya tumbo.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kinywa kikavu na kuzuilika kwa mkojo.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[1] Dawa hii ni dawa za antihistamini, yaani dawa zinazotumika kupunguza dalili za mzio (antihistamine).[1]

Carbinoxamine ilipewa hati miliki mwaka wa 1947 na ilianza kutumika katika matibabu mwaka wa 1953 [2] na inapatikana kama dawa ya kawaida.[3] Nchini Marekani, vidonge 60 vya miligramu 4 hugharimu takriban dola 20 kufikia mwaka wa 2021.[3]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Carbinoxamine Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 30 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Fischer J, Ganellin CR (2006). Analogue-based Drug Discovery (kwa Kiingereza). John Wiley & Sons. uk. 545. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-10-31. Iliwekwa mnamo 2021-01-26.
  3. 3.0 3.1 "Carbinoxamine Maleate Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Agosti 2016. Iliwekwa mnamo 30 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Carbinoxamine kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.