Caroline Reynolds
Caroline Reynolds ni jina la kutaja uhusika wa katika kipindi cha televisheni cha Kimarekani, maarufu kama Prison Break. Uhusika huu ulichezwa na Patricia Wettig.
Uhusika wa Prison Break | |
---|---|
Caroline Reynolds | |
Caroline Reynolds | |
Mwonekano wa kwanza: | Allen |
Msimu: | 1,2
Sehemu Alizocheza = 18 |
Imechezwa na: | Patricia Wettig |
Kazi yake: | Rais wa zamani wa 46 wath Marekani ; Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani ; Seneta wa zamani wa Jimbo la Illinois |
Familia: | Terrence Steadman (kaka yake, amekufa), ana wajukuu kadhaa |
Mahusiano: | Paul Kellerman |
Alianza kuonekana katika sehemu ya pili ya mfululizo akiwa kama mwanamke wa mafumbo (maranyingi alionekana akiulizia kazi) ambaye sura yake haikuonekana hadi ilipofikia sehemu ya nane ya mfululizo huu, ambapo aligundulika kuwa alikuwa Makamu wa Rais wa Marekani ndiye aliyekuwa akifanya hivyo.
Kaka yake, Terrence Steadman, ni mtu ambaye inasemekana Lincoln Burrows alifungwa kwa kumwua. Reynolds akawa maarufu zaidi, akaja kuwa adui mkubwa wa msimu wa kwanza.
Katika msimu wa kwanza, Reynolds alishirikiana na jumuia ya washenzi ijulikanayo kama "The Company" ambao alikuwa alishirikiana nao kuhakikisha lengo lao la kumpoteza Lincoln Burrows limekamilika kwa kisingizio cha kumwua kaka wa makamu wa Rais.