Chama cha Walimu Tanzania

chama cha muungano wa walimu Tanzania

Chama cha Walimu Tanzania ni chama cha wafanyakazi walio walimu nchini Tanzania.

Historia hariri

Chama cha walimu kiliundwa mnamo mwaka 1993 kwa nia ya kutetea na kukuza haki za walimu nchini Tanzania.

Mnamo mwaka 2006, rais wa umoja huo Margaret Simwanza Sitta aliteuliwa na Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi. [1]

Mnamo mwaka wa 2012, walimu 200,000 waligoma baada ya asilimia 95.7 ya wanachama wa Muungano walipiga kura. Mwenyekiti wa Umoja huo Gratian Mukoba alisema kuwa ongezeko la mshahara lilikuwa muhimu.[2]

Mnamo Mei 2017, umoja huo ulilaani kufutwa kazi kwa wafanyikazi wa serikali 10,000.[3]

Uongozi hariri

Leah Ulaya ndiye rais wa sasa wa umoja wa walimu nchini Tanzania. [4] Christopher Banda ni Makamu wa Rais. Ezekiah Oluoch alikuwa naibu katibu mkuu. [5] [6]

Marejeo hariri