Chamkano

ukarasa wa maana wa Wikimedia

Chamkano (ing. Ilihifadhiwa 24 Machi 2015 kwenye Wayback Machine. fraction) ni namna ya kutaja sehemu sawa za jumla fulani katika lugha ya hisabati.

Machamkano ya nusu na robo kwa mfano wa keki

Mifano ya machamkano katika maisha ya kawaida ni nusu, theluthi, robo. Tunaweza kutaja theluthi mbili, robo mbili ambayo ni sawa na nusu au robo tatu.

Chamkano huandikwa kwa tarakimu ya kuhesabu inayoandikwa juu ya mstari na tarakimu za kutaja idadi ya sehemu zinazoandikwa chini ya mstari:

  • au 1/2 = nusu moja
  • au 3/4 = robo tatu
  • au 17/3 = kumi na saba theluthi
  • au 10/12 = kumi za kumi na mbili