Changarawe
Changarawe ni mawe madogo. Kama ukubwa wa kila kijiwe ni chini ya 2 mm ndipo mchanga. Kama ni kubwa zaidi kuliko 60-75 mm (kawaida hutofautiana kati ya nchi na nchi) si changarawe tena ni jiwe.
Changarawe imetokea kutokana na mmomonyoko wa mawe au mwamba. Idadi kubwa ya changarawe hutokana na mmomonyoko katika mito. Njia nyingine ni mmomonyoko wa barafuto.
Changarawe inapatikana pia kama miamba au mawe makubwa yanaanguka mlimani na kupasuka.
Changarawe ni jambo muhimu katika ujenzi. Kama kokoto inatumika chini ya barabara au kuchanganywa na simiti kwa ajili ya misingi ya majengo.