Chanzo (mto)
Chanzo cha mto ni mahali ambako mto huu unaanza. Mara nyingi ni chemchemi yaani mahali ambako maji yaliyokusanyika chini ya ardhi yanatoka nje na kuonekana kwenye uso wa ardhi.
Kwa mito mingine inaweza kuwa mahali ambako mito miwili inaungana na watu wameamua kupatazama kama mto mpya unaanza hasa kama mito asilia haina tofauti sana katika ukubwa wao kwa hiyo haiwezekani kusema mto mmoja unaingia katika mto mwingine. Mfano ni mto Weser katika Ujerumani.
Chanzo cha mto ni pia mahali ambako mto unatoka katika ziwa kwa mfano mto wa Naili unapotoka katika Ziwa Viktoria.