Chekehukwa
Chekehukwa wa Ulaya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Charadriiformes (Ndege kama makorongo)
Familia: Burhinidae (Ndege walio na mnasaba na chekehukwa)
Jenasi: Burhinus Illiger, 1811

Esacus Lesson, 1831

Chekehukwa ni ndege wa familia ya Burhinidae.

Ndege hao wana rangi zinazowanyerereza wakisimama au kutembea chini. Wakiona hatari husimama tuli na hupatana na mahali pa nyuma. Kwa hvyo hawaonekani sana wakati wa mchana. Huenda zaidi usiku na huonekana mara kwa mara mwangani kwa mbele kwa gari. Husikika zaidi ya kuoneka.

Wanatokea maeneo makavu na hula wadudu, mijusi na wanyama wadogo.

Spishi za Afrika (na Ulaya) hariri

Spishi za mabara mengine hariri

Picha hariri