Choo cha shimo
Choo cha shimo au choo cha zamani ni aina ya choo ambapo kinyesi cha binadamu hukusanywa kwenye shimo ardhini.
Ufasili na manufaa
haririVyoo hivi havitumii maji au hutumia kati ya lita moja na tatu kwa kila mara ya utumiaji kwa vyoo vya shimo vinavyotumia maji ya kumwangwa.[2] Vikijengwa na kudumishwa vyema, vinaweza kupunguza kuenea kwa magonjwa kwa kupunguza kiasi cha kinyesi cha binadamu kwenye mazingira kutokana na kwenda choo mahali wazi.[3][4] Hii hupungza usambazaji wa vimelea kutoka kwa kinyesi hadi chakula unaosababishwa na nzi.[3] Vimelea hivi ni visababishi vikuu vya maambukizi ya kuharisha na maambukizi wa minyoo ya utumbo.[4] Maambukizi ya kuharisha yalisababisha takriban vifo milioni 0.7 vya watoto wa umri wa chini ya miaka mitano mwaka wa 2011 na watoto milioni 250 walikosa kwenda shuleni siku kadhaa.[4][5] Vyoo vya mashimo ni mbinu ya gharama ya chini zaidi ya kuhakikisha kinyesi kimeondolewa karibu na watu.[3]
Ujenzi na uondoaji kinyesi
haririKwa kijumla, choo cha shimo huwa na sehemu tatu: shimo la ardhini, sakafu iliyo na shimo dogo, na chumba kilicho na paa.[2] Kwa kawaida, shimo la ardhini huwa na kina cha angalau mita 3 (futi 10 ) na upana wa mita 1 (futi 3.2).[2] Shirika la Afya Duniani kinapendekeza vijengwe mbali kidogo na nyumba, kwa kuzingatia masuala ya harufu inayotoka chooni na ufikiaji wa urahisi.[3] Umbali na maji ya ndani ya ardhi na maji ya juu ya ardhi unafaa kuwa mkubwa iwezekanavyo ili kupunguza hatari ya uchafuzi. Shimo la sakafuni halifai kuzidi upana wa sentimita 25 (inchi 9.8) ili watoto wasije wakaanguka humo. Mwangaza haufai kuingia humo ili kuzuia inzi wasiingie. Jambo hili linaweza kuhitaji kutumia kifuniko kwenye shimo la sakafuni ikiwa halitumiki.[3] Choo kikishajaa hadi mita 0.5 (futi 1.6) karibu na sehemu ya juu, kinafaa kuondolewa kinyesi chote au choo kipya kijengwe mahali tofauti.[6] Udhibiti wa maji maji ya kinyesi yaliyoondolewa chooni huwa tata. Kuna hatari za kimazingira na kiafya yasipodhibitiwa vyema.
Uboreshaji
haririChoo cha shimo cha kawaida kinaweza kuboreshwa kwa njia kadhaa. Njia ya kwanza ni kuweka mfereji wa kuingiza hewa shimoni hadi juu ya mjengo wa choo. Mfereji huu huboresha uzungukaji wa hewa na kupunguza harufu mbaya ya choo. Pia unaweza kupunguza nzi ikiwa sehemu ya juu ya mfereji huu imefunikwa kwa waya (ambayo kwa kawaida huwa imetengenezwa kwa kioo nyuzi). Katika aina hii ya vyoo, si lazima kifuniko kitumike kufunika shimo la sakafuni.[6] Hatua zingine za uboreshaji zinazoweza kutumika ni pamoja na sakafu iliyojengwa kwa njia inayowezesha maji kutiririkia ndani na kuimarisha sehemu ya juu ya sakafu kwa matofali au simiti ili kuongeza uthabiti.[2][6]
Utumizi, Jamii na Utamaduni
haririKufikia mwaka wa 2013, vyoo vya shimo vinatumiwa na takriban watu bilioni 1.77.[7] Hii ni hasa katika mataifa yanayostawi na pia maeneo ya mashambani na majagwa. Mwaka wa 2011, takriban watu milioni 2.5 hawakuwa na vyoo vizuri na watu milioni moja walilazimika kwenda choo katika sehem wazi katika mazingira yao.[8] Kaskazini mwa Asia na Mataifa ya Kusini mwa Sahara yalikuwa na ufikiaji duni zaidi wa vyoo.[8] Katika mataifa yanayostawi, gharama ya choo kidogo kwa kawaida ni kati ya dola 25 na 60 za Marekani.[9] Gharama za kuendelea kuviboresha ni kati ya dola 1.5 na 4 za Marekani kwa kila mtu kwa mwaka, ambazo mara nyingi hazitiliwi maanani.[10] Katika baadhi ya sehemu za mashambani mwa India kampeni ya "Hamna Choo, Hamna Ndoa" imetumika kuhamasisha umma kuhusu vyoo kwa kuwahimiza wanawake wakatae kuolewa na mwanaume asiye na choo.[11][12]
References
hariri- ↑ WEDC. Latrine slabs: an engineer’s guide, WEDC Guide 005 (PDF). Water, Engineering and Development Centre The John Pickford Building School of Civil and Building Engineering Loughborough University. uk. 22. ISBN 978 1 84380 143 6.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 Tilley, E., Ulrich, L., Lüthi, C., Reymond, Ph. and Zurbrügg, C. (2014). Compendium of Sanitation Systems and Technologies (tol. la 2). Dübendorf, Switzerland: Swiss Federal Institute of Aquatic Science and Technology (Eawag). ISBN 9783906484570.
{{cite book}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 "Simple pit latrine (fact sheet 3.4)". who.int. 1996. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-12-19. Iliwekwa mnamo 15 Agosti 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 4.2 "Call to action on sanitation" (PDF). United Nations. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (pdf) mnamo 2014-08-19. Iliwekwa mnamo 15 Agosti 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Walker, CL; Rudan, I; Liu, L; Nair, H; Theodoratou, E; Bhutta, ZA; O'Brien, KL; Campbell, H; Black, RE (Apr 20, 2013). "Global burden of childhood pneumonia and diarrhoea". Lancet. 381 (9875): 1405–16. doi:10.1016/s0140-6736(13)60222-6. PMID 23582727.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 6.0 6.1 6.2 François Brikké (2003). Linking technology choice with operation and maintenance in the context of community water supply and sanitation (PDF). World Health Organization. uk. 108. ISBN 9241562153. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2005-11-05. Iliwekwa mnamo 2015-08-17.
- ↑ Graham, JP; Polizzotto, ML (Mei 2013). "Pit latrines and their impacts on groundwater quality: a systematic review". Environmental health perspectives. 121 (5): 521–30. doi:10.1289/ehp.1206028. PMID 23518813.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 8.0 8.1 Progress on sanitation and drinking-water - 2014 update (PDF). WHO. 2014. ku. 16–20. ISBN 9789241507240. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (pdf) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2015-08-17.
{{cite book}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ Selendy, Janine M. H. (2011). Water and sanitation-related diseases and the environment challenges, interventions, and preventive measures. Hoboken, N.J.: Wiley-Blackwell. uk. 25. ISBN 9781118148600.
- ↑ Sanitation and Hygiene in Africa Where Do We Stand?. Intl Water Assn. 2013. uk. 161. ISBN 9781780405414.
- ↑ Global Problems, Smart Solutions: Costs and Benefits. Cambridge University Press. 2013. uk. 623. ISBN 9781107435247.
- ↑ Stopnitzky, Yaniv (12 Desemba 2011). "Haryana's scarce women tell potential suitors: "No loo, no I do"". Development Impact. Blog of World Bank. Iliwekwa mnamo 17 Novemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)