Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN) ni chuo kikuu kikubwa zaidi nchini Kenya. Ingawa historia yake kama taasisi ya elimu ilianza 1956, hakikufanya kuwa chuo kikuu huria mpaka 1970 wakati Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki kiligawanywa katika vyuo vikuu huria: Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania, na Chuo Kikuu cha Nairobi.

Chuo Kikuu cha Nairobi
University of Nairobi
Kimeanzishwa1956 Royal Technical College
1961 Royal College Nairobi
1964 University College Nairobi
1970 University of Nairobi
AinaPublic
ChanselaJoseph Barrage Wanjui
Wanafunzi wa
shahada ya kwanza
17,200
Wanafunzi wa
uzamili
4,800
MahaliNairobi, Kenya
KampasiMjini
AffiliationsACU
Tovutiwww.uonbi.ac.ke
Chuo kikuu cha Nirobi

Mwaka wa 2002 Chuo hiki kilikuwa na wanafunzi 22,000, na 17,200 kati yao walikuwa wakisomea shahada ya msingi na 4,800 walikuwa wakisomea shahada ya kumudu. Chuo kikuu kimezindua mipango kadhaa ya kisera na kuanzisha shahada sambamba kukabiliana na mahitaji ya elimu nchini Kenya.

Historia

Mwanzo wa Chuo Kikuu cha Nairobi huanzia 1956, pamoja na uanzishwaji wa Royal Technical College ambapo walisajili kundi la kwanza la wahitimu wa masomo ya A-levels katika masomo ya kiufundi mwezi wa Aprili mwaka huo huo. Royal Technical College ilibadilishwa kuwa Chuo cha pili katika Afrika Mashariki tarehe 25 Juni 1961 chini ya jina Royal College Nairobi. Chuo kilikuwa na uhusiano maalum na Chuo Kikuu cha London ambapo kilianza kuandaa wanafunzi katika vitivo ya sanaa, sayansi, na uhandisi kwa tuzo ya shahada kutoka Chuo Kikuu cha London.

Tarehe 20 Mei 1964, Royal College Nairobi ilibadilishwa jina ikawa University College Nairobi kama chuo kilichokuwa sehemu ya Inter-territorial Federal University of East Africa, na baadaye vizazi ya wanafunzi waliojiunga walikuwa wakihitimu shahada zao kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki badala ya Chuo Kikuu cha London. Mwaka 1970, University College Nairobi kiligeuzwa kikawa chuo kikuu cha Taifa cha kwanza nchini Kenya na kikabadilishwa jina kuwa Chuo Kikuu cha Nairobi.

Hivi majuzi, chuo kikuu kimefanya mahusiano na Chuo Kikuu cha Rome La Sapienza na Vrije Universiteit Brussel huko Ubelgiji hasa kwa madhumuni ya utafiti.

Vyuo

Kwa mtazamo wa upanuzi wa haraka na ugomo wa utawala, chuo kikuu kilifanywa marekebishaji mwaka 1983 kusababisha mgawanyiko wa utawala kupitia uumbaji wa vyuo vya kampasi sita zinazoongozwa na wakuu.

  • Chuo cha Kilimo na Afya ya Wanyama (Kampasi ya Kabete Kaskazini)
  • Chuo cha Usanifu na Uhandisi (Kampasi Kuu)
  • Chuo cha Biolojia na Sayansi za Kimwili (Kampasi ya Chiromo)
  • Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Nje (Kampasi ya Kikuyu)
  • Chuo cha Sayansi ya Afya (Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta)
  • Chuo cha Utu na Sayansi ya Kijamii (Kampasi Kuu)

Vitivo

  • Kitivo cha Kilimo
  • Kitivo cha Sanaa
  • Kitivo cha Biashara (Faculty of Commerce)
  • Kitivo cha Elimu
  • Kitivo cha Masomo ya Nje
  • Kitivo cha Sheria
  • Kitivo cha Sayansi
  • Kitivo cha Sayansi ya Kijamii
  • Kitivo cha Afya ya Wanyama
  • Taasisi ya Masomo ya Kiafrika
  • Shule ya kompyuta na data
  • Shule ya Uhandisi
  • shule ya Sayansi ya Uuguzi
  • Shule ya Sayansi ya Meno
  • Shule ya Utabibu
  • Shule ya Madawa
  • Shule ya Mazingira yaliyojengwa

Viungo vya nje

1°16.78′S 36°48.99′E / 1.27967°S 36.81650°E / -1.27967; 36.81650

  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Nairobi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.