Chuo cha Kimataifa cha Britania Kairo
shule huko New Cairo, Misri
Chuo cha Kimataifa cha Britania Kairo (BICC) ni shule ya awali, shule ya msingi na shule ya sekondari iliyoko Wilaya ya Tano huko New Cairo, Misri.[1]
Kampasi ya chuo ina takribani wanafunzi 800 kutoka darasa la awali hadi mwaka wa 12. Imejengwa kwenye eneo la mita za mraba 7,000, shule ina miundombinu mizuri na ya kisasa ikiwa na madarasa 42, maabara 3, na madarasa 8 ya shughuli mbalimbali. Shule ina uwiano wa wanafunzi kwa mwalimu wa 11:1.
Chuo cha Kimataifa cha Britania Kairo kinawajengea wanafunzi maisha. BICC inatoa elimu ya Britania.