Kekeo

Ndege vidusia wa familia Cuculidae
(Elekezwa kutoka Clamator)
Kekeo
Kekeo kidari-chekundu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Cuculiformes (Ndege kama kekeo)
Familia: Cuculidae (Ndege walio na mnasaba na kekeo)
Nusufamilia: Cuculinae (Ndege wanaofanana na kekeo)
Ngazi za chini

Jenasi 12:

Kekeo ni ndege wadogo hadi wakubwa kiasi wa nusufamilia Cuculinae katika familia Cuculidae. Wana mkia mrefu na mabawa marefu na membamba. Miguu yao ina vidole viwili vikabilivyo mbele na viwili vikabilivyo nyuma. Rangi zao kuu ni nyeusi, nyeupe na rangi ya kijivi, pengine rangi ya majani na ya manjano. Kekeo hula wadudu, mabuu ya wadudu na matunda, na spishi kubwa hula wanyama wadogo pia.

Kekeo hawajengi tago lao lenyewe lakini hutaga mayai yao katika matago ya ndege wengine, yai moja katika kila tago baada ya kutoa yai moja la mwenye tago (udusio wa kiota, Kiing. brood parasitism). Kwa kawaida mayai ya kekeo yafanana na yale ya mwenye tago. Mara nyingi ndani ya domo la makinda yao ni sawasawa na ile ya makinda ya mwenyewe, pengine wanafanana kabisa, lakini kinda la kekeo ni takriban kila mara mkubwa zaidi. Akitoka yai ayasukuma mayai au makinda ya mwenyewe nje ya tago. Mwenye tago aendelea kumpa kinda la kekeo chakula.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za Asia

hariri

Spishi za kabla ya historia

hariri
  • Eocuculus sp. - (Mwisho wa Eocene ya Teller County, MMA)
  • Eudynamis cf. taitensis (Henderson Island Koel) (Mwisho wa Quaternary)