Cri-Zelda Brits
Mcheza kriketi wa Afrika Kusini
Cri-Zelda Brits (pia Crizelda Brits, * 20 Novemba 1983) ni mchezaji wa kriketi wa kimataifa kutoka Afrika Kusini akirusha kwa mkono wa kulia.
Cri-Zelda Brits | |
Nchi | Afrika Kusini] |
---|---|
Kazi yake | Mchezaji wa kriketi |
Brits aliingia mara ya kwanza katika timu ya wanawake wa kitaifa ya kriketi kama "bowler" (mtupa mpira) wa kwanza mwaka 2002. Aliendelea kushika nafasi mbalimbali na tangu 2005 kuwa hodari zaidi upande wa "“batter”" (kupiga mpira kwa fimbo). Aliongoza timu katika mechi 23 katika miaka ya 2007 na 2008, tena mwaka 2011 kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ya 2010.
Anatazamiwa kuwa kati ya wachazaji wanawake bora wa kriketi katika Afrika Kusini.