Jinai

(Elekezwa kutoka Crime)

Jinai ni kitendo kinachofanywa na mtu ambacho ni kinyume sana na sheria za nchi au eneo. Kwa hiyo jinai inafafanuliwa na sheria inayotaja matendo maalum kuwa vile[1].

Matendo yanayotajwa kama jinai hutazamwa kuwa hatari kwa amani katika jamii na pia kuvunja haki za watu. Kwa hiyo katika mifumo ya sheria ya kisasa dola linalenga kulinda amani na haki kwa kutunga sheria zinazokataza jinai. Kwa hiyo si kazi ya mtu aliyepata madhara kufuatilia jinai, bali ni kazi ya dola.[2]

Kwa kawaida tendo fulani linahitaji kutendwa pamoja na nia ya kuvunja sheria ili kutajwa kama jinai. Hata hivyo, pia matendo maalum yanayotendwa "kwa namna ya kutokuwa mwangalifu au kupuuza kwa kiasi cha kuhatarisha maisha ya binadamu au kusababisha dhara kwa mtu mwingine yeyote"[3] yanaweza kuangaliwa kama jinai.

Ilhali kila jinai inavunja sheria, siyo kila uvunjaji wa sheria unahesabiwa kama jinai. Kuvunja sheria za biashara na mikataba baina ya watu inaweza kufuatiliwa kwa kesi za madai mbele ya mahakama, lakini mara nyingi hazifuatiliwi mara moja na vyombo vya dola.

Kutokea kwa jinai kunahitaji kuthibitishwa na mahakama au jaji anayeangalia mashtaka dhidi ya mtu na kutoa hukumu ambako hatia fulani kulingana na sheria inathibitishwa au kukataliwa. Kama mkosaji anahukumiwa kuwa na hatia, jaji ataamua kuhusu adhabu yake. Sheria za jinai hutaja adhabu maalumu kwa kila aina ya kosa, ilhali jaji kwa kawaida ana chaguo fulani kuamulia kiwango cha adhabu.

Marejeo hariri

  1. [https://sheriakiganjani.co.tz/page.php?key=226 Nini maana ya jinai?], tovuti ya Sheria Kiganjani, inayotolewa na Tanganyika Law Society
  2. Wakili Manace Ndoroma: Kosa la jinai, maelezo na ufafanuzi
  3. Kanuni ya Adhabu Tanzania (Penal Code , Chapter 16 of the Laws (revised), Jinai kwa kutojali na kupuuza, ss. 233.

Kujisomea hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jinai kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.