David Gallagher
David Lee Gallagher (alizaliwa Februari 9, 1985) ni mwigizaji na mwanamitindo wa zamani kutoka Marekani. Alianza kazi yake akiwa mtoto mdogo katika uigizaji na mitindo akiwa na umri wa miaka miwili. Gallagher ameteuliwa mara tano kwa Tuzo za Msanii Chipukizi (Young Artist Award) na pia ameshinda Tuzo ya Teen Choice. Anajulikana zaidi kwa kuigiza kama Mikey Ubriacco katika Look Who's Talking Now na Simon Camden kwenye 7th Heaven. Pia aliigiza kama Kevin Harper katika Angels in the Endzone na Richie Rich katika Richie Rich's Christmas Wish. Gallagher pia anajulikana sana kwa kutoa sauti ya mhusika Riku katika mfululizo wa michezo ya video ya Kingdom Hearts.[1]
Marejeo
hariri- ↑ St. John, Warren. "Making Sure Hollywood's Nouveau Riche Stay Riche", August 22, 2004, p. 9009001.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu David Gallagher kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |