David Woodard

mwandishi Mmarekani na muongozaji

David Woodard (alizaliwa Aprili 6, 1964) ni mwandishi Mmarekani na muongozaji. Wakati wa miaka ya 1990 alitunga neno “prequiem”, ambalo ni muunganiko kati ya maneno “preemptive” na “requiem”, ili kuelezea ushiriki wake wa Kibuddha wa kutunga nyimbo maalumu za kuchezwa wakati wa au muda kidogo kabla ya kifo cha kiumbe.[1][2]

Woodard, 2020

Huduma za ukumbusho wa kifo zinazopatikana Los Angeles ambapo Woodard alitumikia kama muongozaji au kiongozi wa muziki ni pamoja na sherehe ya kiraia ya mwaka 2001 katika uwanja wa ndege ambao hautumiki na sasa ni reli ya Angels Flight wakikumbuka ajali iliyosababisha kifo cha Leon Praport na kumjeruhi mjane Lola.[3][4]: 125  Amefanya “prequiem” kwa Wanyama pori, kwa ajili ya California Brown Pelician katika eneo la pwani pembezoni mwa ufukwe mahali ambapo mnyama alifia.[5]

Woodard anajulikana kwa kutengeneza chombo kinachofanana na Dreamachine, taa yenye athari za kisaikolojia, ambayo imeonyeshwa katika makumbusho ya Sanaa duniani kote. Huko Ujerumani na Nepal anajulikana kwa michango yake kwenye jarida la fasihi la Der Freund, ikiwemo machapisho yake juu ya karma kwa jamii mbalimbali za viumbe, ufahamu wa mimea na makazi ya Waparaguay Nueva Germania.[6]

Woodard alisoma katika chuo cha The New School for Social Research, na Chuo Kikuu cha California, Santa Barbara (UCSB).[7]

Nueva Germania

hariri

Mnamo mwaka 2003 Woodard aliteuliwa kuwa mjumbe wa baraza huko Juniper Hills (Los Angeles Vijijini), California. Katika nafasi hii alipendekeza uhusiano na mji wa Nueva Germania, Paraguay. Ili kuendeleza mpango wake, Woodard alisafiri kuelekea eneo lililokuwa ni sehemu iliyopendwa na watu wanaokula mboga za majani tu / watetezi wa haki za wanawake na kukutana na uongozi wa manispaa. Kufuatia ziara yake ya kwanza, alichagua kuachana na mpango huo wa kutafuta uhusiano lakini katika jumuiya hiyo alipata kitu cha kujifunza kwa ajili ya machapisho ya baadae. Kitu ambacho kilimvutia ni mawazo ya kiproto-transhumanist ya waliobashiriwa kuwa waandaaji Richard Wagner na Elisabeth Förster-Nietzsche, ambaye pamoja na mume wake Bernhard Förster walianzisha na waliishi katika koloni kati ya 1886 na 1889.[7]

 
Woodard na Burroughs nyuma ya Dreamachine, mnamo 1997[8]: 98–101 

Kuanzia mwaka 2004 mpaka 2006 Woodard aliongoza safari nyingi kwenda Nueva Germania, akipata msaada kutoka kwa aliyekuwa Makamu wa Raisi wa Marekani Dick Cheney.[9] Mwaka 2011 Woodard alimpatia ruhusa mwandika riwaya wa Uswisi Christian Kracht ya kuchapisha mahusiano yao ya kawaida, mengi yakihusisha Nueva Germania,[10]: 113–138  kwa matoleo mawili chini ya Chuo cha Hannover imprint Wehrhahn Verlag.[11]: 180–189  Katika mabadilishano ya barua, Frankfurter Allgemeine Zeitung anasema, "[Waandishi] wamevunja mipaka iliyopo kati ya maisha na sanaa.”[12] Der Spiegel anapendekeza kwamba toleo la kwanza, Five Years,[13] ni “kazi iliyoandaliwa kiroho” kwa riwaya ya Kracht iliyofuata ya Imperium.[14]

Kwa mujibu wa Andrew McCann, Woodard alijitosa kwenye “safari ya kwenda kwenye kilichobaki, mahali ambapo wakazi asili wa kwanza waliishi katika hali ngumu kimaisha” na kuendelea kwenda “kukuza zaidi mambo ya asili ya jamii, na pia kujenga nyumba ndogo kama ya Bayreuth ya opera katika eneo ambalo kwa kipindi fulani familia ya Elisabeth Förster-Nietzsche iliishi.”[15][n 1] Katika miaka ya hivi karibuni Nueva Germania imebadilika na kuwa sehemu ya kutembelea, ikiwa na kitanda na chakula cha asubuhi na makumbusho ya kihistoria.

Dreamachine

hariri

Kuanzia mwaka 1989 mpaka 2007 Woodard alitengeneza mfano wa Dreamachine,[16][17] mashine inayowakawaka mwanga iliyobuniwa na Brion Gysin na Ian Sommerville ambayo ina silinda iliyo wazi, iliyotengenezwa na madini ya shaba au karatasi, ikizunguka taa ya umeme—inapotazamwa na macho yaliyofungwa mashine hii inaweza kusababisha hisia za kifikra zinazoweza kufanana na kuleweshwa na madawa au kuota.[18][n 2]

Baada ya kuchangia Dreamachine kwa William S. Burroughs katika maonyesho ya LACMA mwaka 1996 Ports of Entry,[19][20] Woodard alijenga urafiki na mwandishi na kumpatia “Bohemian model” (karatasi) ya Dreamachini kama zawadi ya sherehe yake ya 83 kuzaliwa ambayo ndiyo ilikuwa ya mwisho.[21][22]: 23  Sotheby's alipiga mnada mashine halisi kwa mnunuzi binafsi mwaka 2002, na nyingine imebakia kama mkopo uliokabidhiwa kutoka kwa Burroughs katika Makumbusho ya Sanaa ya Spencer.[23]

Marejeo na vidokezo

hariri

Vidokezo

hariri
  1. Mwanafiziolojia wa zamani kutoka Uswisi Thomas Schmidt anaifananisha sauti ya kiuandishi ya Woodard na sauti ya mshiriki aliyekuwa katika mandhari ya nyuma ndani ya riwaya ya Thomas Pynchon.
  2. Katika mwaka 1990 Woodard alivumbua mashine bandia ya kuathiri fikra, Feraliminal Lycanthropizer, athari ambazo zinasemekana ni kinyume na zile za Dreamachine.

Marejeo

hariri
  1. Carpenter, S., "In Concert at a Killer's Death", Los Angeles Times, Mei 9, 2001.
  2. Rapping, A., Picha ya Woodard (Seattle: Getty Images, 2001).
  3. Reich, K., "Family to Sue City, Firms Over Angels Flight Death", Los Angeles Times, Machi 16, 2001.
  4. Dawson, J., Los Angeles' Angels Flight (Mount Pleasant: Arcadia Publishing, 2008), ukurasa 125.
  5. Manzer, T., "Pelican's Goodbye is a Sad Song", Press-Telegram, Oktoba 2, 1998.
  6. Carozzi, I., "La storia di Nueva Germania", Il Post, Oktoba 13, 2011.
  7. 7.0 7.1 Riniker, C., "Autorschaftsinszenierung und Diskursstörungen in Five Years", katika J. Bolton, et al., wahariri, German Monitor 79 (Leiden: Brill, 2016).
  8. Chandarlapaty, R., "Woodard and Renewed Intellectual Possibilities", katika Seeing the Beat Generation (Jefferson, NC: McFarland & Company, 2019), kurasa 98–101.
  9. Epstein, J., "Rebuilding a Home in the Jungle" Archived 9 Oktoba 2016 at the Wayback Machine., San Francisco Chronicle, Machi 13, 2005.
  10. Schröter, J., "Interpretive Problems with Author, Self-Fashioning and Narrator", katika Birke, Köppe, wahariri, Author and Narrator (Berlin: De Gruyter, 2015), kurasa 113–138.
  11. Woodard, D., "In Media Res", 032c, Majira ya joto 2011, kurasa 180–189.
  12. Link, M., "Wie der Gin zum Tonic", Frankfurter Allgemeine Zeitung, Novemba 9, 2011.
  13. Kracht, C., & Woodard, Five Years (Hannover: Wehrhahn Verlag, 2011).
  14. Diez, G., "Die Methode Kracht", Der Spiegel, Februari 13, 2012.
  15. McCann, A. L., "Allegory and the German (Half) Century" Archived 9 Oktoba 2016 at the Wayback Machine., Sydney Review of Books, Agosti 28, 2015.
  16. Allen, M., "Décor by Timothy Leary", The New York Times, Januari 20, 2005.
  17. Stirt, J. A., "Brion Gysin's Dreamachine—still legal, but not for long", bookofjoe, Januari 28, 2005.
  18. Woodard, maandishi ya maonyesho, Program, Berlin, November 2006.
  19. Knight, C., "The Art of Randomness", Los Angeles Times, Agosti 1, 1996.
  20. Bolles, D., "Dream Weaver", LA Weekly, Julai 26–Agosti 1, 1996.
  21. Ubalozi wa Marekani, Prague, "Literární večer s diskusí", Oktoba 2014.
  22. Woodard, "Burroughs und der Steinbock", Schweizer Monat, Machi 2014, ukurasa 23.
  23. Makumbusho ya Sanaa ya Spencer, Dreamachine, Chuo Kikuu cha Kansas.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: