Madawa ya kulevya

(Elekezwa kutoka Dawa za kulevya)

Madawa ya kulevya ni hatari sana kwa binadamu kwa kuwa husababisha magonjwa kama mapafu na kuharibu utindio wa ubongo.

Aina mbalimbali ya madawa ya kulevya.

Mfano wa madawa hayo ni kama kokaini, heroini, bangi na miraa.

Kuna watu wengi walioathiriwa na madawa ya kulevya, lakini yanazidi kuenea kwa sababu ni biashara kubwa inayoingiza pesa nyingi.

Serikali inatakiwa kutoa elimu kuhusiana na madhara yatokanayo na matumizi ya madawa ya kulevya, kwani ni hatari kwa maisha ya binadamu na kwa jamii.

Mara chache yanaweza kusaidia wagonjwa kwa kuwafanya wasisikie maumivu makali mno.

Ulevi wa madawa ya kulevya

Dawa za kulevya hutumiwa kwa njia nyingi ikiwemo kuvuta kama sigara na bangi, kula kama peremende, kumeza kama tembe, kunusia hasa zile dawa za kulevya ungaunga, kunywa kwa zile dawa za kulevya majimaji, au kutafuna na kumeza maji yake kisha kutupa mabaki kama vile miraa. Dawa nyingine hutumiwa kwa njia ya kupikia chakula au vinywaji kama viungo, kujindunga sidano na kupumua mivuke yake ijulikanayo kwa lugha za kimsimu kama "dabbing"

Utumizi wa madawa ya kulevya hufanya mtumiaji alewe na ajisikie huru au kuwa upeo mwingine kuliko wa kawaida. Katika lugha za kimsimu huitwa kuwa ‘high’ au ‘stoned’. Hali hii humfanya mtu awe mtovu wa nidhamu au kufanya mambo ambayo hata mwenyewe atashtuka baadaye akiwa hajatumia madawa.

Pia utumizi huu huathiri mtu kiafya. Kwa mfano ukitumia bangi, utapata kwamba moyo wako wadunda haraka kuliko kawaida, kinywa chako chakauka, macho kuwa mekundu, kusahau kwa haraka na kupata uchu mkubwa wa chakula. Uvutaji wa bangi pia huathiri mapafu, ini na ubongo kufikia hata kuwa mwendawazimu.

Wanawake wajawazito wanapovuta au kutumia bangi huenda wakaavya mimba bila kukusudia, mtoto kuwa hajakomaa vizuri hata wakati wa kuzaliwa.

Udhibiti wa madawa ya kulevya

Serikali za nchi nyingi zimedhibiti au hata kupiga marufuku utumiaji wa madawa ya kulevya. Mwakani 1960, kulikuwa na udhibiti wa upanzi wa bangi wa kimataifa.

Nchi nyingine zinaruhusu upanzi na utumizi wa madawa hayo kwa minajili ya matibabu. Kwa mfano bangi inatumika katika kupunguza maumivu ya wagonjwa wa saratani na kuwapa uchu wa chakula wanaokisusua. Heroini ambayo inatokana na dawa ya mofini hutumika katika kupunguza maumivu kwa wagonjwa wa saratani pia.

Matibabu baada ya uraibu wa madawa ya kulevya

Walioathirika na utumizi wa madawa ya kulevya huweza kunasuliwa kutoka uraibu ule katika vituo maalumu. Huku, wao huonyeshwa jinsi ya kuishi bila kutumia madawa. Pia wanapewa dawa nyingine zinazowasaidia waache uchu wa madawa ya kulevya.

Tanbihi


Viungo vya nje

  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Madawa ya kulevya kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.